Amber Lulu Awafunda Wanaotafuta Umaarufu Mitandaoni

Mrembo anayepamba video za wasanii bongo ‘ Amber Lulu amewataka warembo wenzake kubadilisha mfumo wa maisha wa kutafuta umaarufu kupitia mitandao ya kijamii kwa kupiga picha zisizofaa na badala yake wafanye kazi za kusaidia jamii ili wakumbukwe.
Image result for Amber Lulu
Akipiga story kwenye Planet Bongo Amber anasema amegundua kuwa kutumia sehemu za miili yao kutafuta umaarufu ni kitu kisicho na maana kwa kuwa umaarufu huo unakuja na kupita kitu ambacho mwisho wa siku watakuwa hawana kitu kipya cha kuonesha kwa mashabiki na kubaki kunyooshewa vidole kwa sababu ya picha hizo wanazotafutia kiki.
“Kutumia maungo kwa ajili ya kutafuta umaarufu siyo mpango kwa kuwa upepo huo utapita halafu tutakuwa hatuna cha kuonesha, bado watoto wa kike tuna mambo mengi ya kufanya kwenye jamii na tukaonekana kuliko kuonesha miili yetu ambapo mwisho wa siku tunadharaulika.” Amesema Amber
Hii siyo mara ya kwanza video vixen huyo kufunguka suala la kuacha sehemu kubwa ya mwili wazi, Wiki iliyopita Ambar Lulu alisema umaarufu wa kuutafutia kwenye mitandao ya kijamii ni kama upepo kwani hutokea na kupita kwa kuwa warembo wapo wengi na kila mmoja anatafuta njia ya kutokea.


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://ift.tt/2ms2574
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


from Blogger http://ift.tt/2nnlLy4
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2m0mHbl
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2mNUW4z
via IFTTT

Related Posts