Nahodha wa Uingereza Wayne Rooney anasema kuwa atasalia katika klabu ya Manchester United baada ya kuhusishwa na uhamisho wa China.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema kuwa anatumai kwamba atashirikishwa kamili katika mechi zilizosalia za klabu hiyo msimu huu.
Mkufunzi wa United Jose Mourinho amekataa kukana kwamba Rooney huenda akaondoka klabu hiyo mwezi huu, ijapokuwa uhamisho huo huenda usikamlike kabla ya kufungwa dirisha la uhamisho nchini China mnamo tarehe 28 Februari.
“Ni wakati wa furaha kubwa katika klabu hii na ningependa kusalia,” alisema Rooney.
Ajenti wake Paul Stretford, alisafiri kuelekea China kuona iwapo arafanikiwa kupata makubaliano, ijapokuwa haijulikani alizungumza na klabu gani.
Mbili kati ya klabu tatu zilizoonekana kuwa klabu m’badala Beijing Guoan na Jiangsu Suning, zilfutilia mbali uvumi kuhusu uhamisho huo.
ANGALIA VIDEO CHIDEO
ANGALIA VIDEO CHIDEO
from Blogger http://ift.tt/2lPtnYm
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2lPLy06
via IFTTT