Wanasayansi waja na Teknolojia ya Kurudisha Watu waliokufa kuwa Hai Tena

Filamu ya Transcendence
Kampuni ya masuala ya utafiti wa kabla na baada ya maisha ya binadamu Humai iliyopo jijini Los Angeles nchini Marekani wanafanyia utafiti na utengenezaji wa teknolojia ambayo itaweza kurudisha watu waliokufa kuwa hai tena kwa kuhamisha ubongo hai wa binadamu na kuupachika katika mwili ambao ni bandia.
‘Nanotechnology, bionics pamoja na artificial intelligence’ ni njia tatu ambazo zitatumika katika kuweza kufanikisha suala hilo ndani ya miaka 30 ili kuweza kuwarudisha binadamu waliokufa kuwa hai tena.
Mwanzilishi wa kampuni hiyo ya Humai, Bwana Josh Bocanegra alisema “Mimi binafsi nakubaliana na kifo, ila sina hofu na kifo. Ila nina uhakika asilimia 100% siku moja nitakufa.” katika ukurasa wa Facebook wa kampuni hiyo pia waliandika kwamba “Hivi kifo sikuzote hakitoepukika? sisi hatufikirii kitu kama hicho.”
Josh Bocanegra alisema kitu kitakacho fanyika ni kuchukua ubongo wa watu waliokufa na kuugandisha ubongo huo kwa kutumia teknolojia maalumu inayoitwa cryonics halafu hapo baadae teknolojia ya kupandikiza ubongo huo kwenye miili bandia itakapokuwa tayari upandikizaji utaanza.
Ubongo uliogandishwa
Josh Bocanera muanzilishi wa Humai
“Kwa kutumia teknolojia hiyo ubongo utaweza kukua sambamba na mwili huo, Mimi sidhani kama ni sawa kifo kituondoe kabisa na kututenganisha na watu ambao tunapendana nao. Nadhani inafika wakati kifo kiwe ni kitu cha ziada kama ukiona umechoka kuishi ila si kiwe kinashindana nasi. Hakuna mtu ambaye anataka kufa, ila nakubaliana na uamuzi wa kila mtu.” alisema Josh Bocanegra ambaye ndiye muanzilishi wa kampuni hiyo ya Humai.
Kitu pekee cha kushangaza kuhusu kampuni hiyi ya Humai ni kwamba inawafanyakazi watano tu, wawili kati yao ni watafiti, mmoja ni balozi na mwingine ni mtaalamu wa masuala ya Artificial Intelligence.
Toa maoni yako hapo chini kuhusu hawa jamaa na hizi teknolojia zao za ajabu zinazotaka kubadilisha ulimwengu.
ANGALIA VIDEO CHIDEO

from Blogger http://ift.tt/2lILehB
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2lID1da
via IFTTT