Isabela Aichezea Sharubu TCRA

MWANAMAMA kutoka kiwanda cha muziki Bongo, Isabela Mpanda anaonekana kuichezea sharubu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ baada ya hivi karibuni kutukana matusi ya nguoni kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram akimtukana shabiki.
Isabela
Isabela alitukana matusi hayo baada ya kuambiwa na shabiki huyo kwamba anawekwa mjinina pedeshee Mtanzania aishiye Uganda, Jack Pemba ambapo mashabiki wake walikerwa na matusi hayo na kuanza kumponda ndipo akaamua kuifuta.
Isabela na Jack Pemba
Akizungumza na Mikito Nusunusu, Isabela alisema alijikuta akitukana baada ya kukerwa na mtu mmoja aliyesema anaendesha maisha kwa kumtegemea Jack Pemba jambo ambalo siyo la kweli.
“Siyo kwamba naichezea sharubu TCRA bali Instagram ndiyo kila kitu siku hizi kwani kuna wengine wanaposti picha wakiwa uchi wa mnyama, nilipatwa na hasira nikaamua nimchane aliyeniambia kwamba nawekwa mjini na Jack Pemba lakini zilipoisha niliyafuta hayo matusi,” alisema.
WAKALI

from Blogger http://ift.tt/2lb7P4F
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2kX0WbK
via IFTTT