RC. DR NCHIMBI: USAFI UWE NI TABIA NJOMBE

Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi aliye vaa kofia ngumu mda mfupi baada ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa usafi kitaifa.

MKUU wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi amepinga wakazi wa mkoa huo kufanya usafi wa mazingira wakati wa kampeni za usafi mazingira kitaifa badara yake usafi kuwa ni tabia.

Dr. Nchimbi anawataka wakazi wa mkoa huo kujijengea tabia ya kufanya usafi mara kwa mara kwenye mazingira yao.

Wito huo aliutoa juzi wakati akikabidhi zawadi kwa halmashauri ya wilaya Njombe, Mji Njombe na vijiji vilivyo ongoza kitaifa mpaka nafasi ya tatu vilivyotoka halmashauri ya wilaya ya Njombe.

Dr. Nchimbi aliwataka wakazi hao kutofanya usafi kwa mazoea na kufanya usafi kama tabia ya wakazi wa Njombe na kusiwe na haja ya watu kuwashindanisha.

Alisema kuwa haiwezekani watu wakawa wanafanya usafi mpaka kuwe na mashindano kitu hicho ni cha hatari kwa kuwa wanaweza kuugua kama hakuta kuwa na mashindano.

Mashindano hayo kitaifa ya usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora mkoa wa Njombe umetwaa ushindi kwa halmashauri zake mbili za Njombe Mji ambayo imepata Pikipiki ambayo imeongoza kwa halmashauri zote za miji nchini.

Halmashauri ya wilaya ya Njombe ikiibuka mshindi kwa halmashauri zote za wilaya nchini na kupata zawadi ya Pikipiki, na Gari moja aina ya Landcruise Hadtop.

Hata hivyo vijiji hapa nchini ushindi uliangukia katika vijiji vya halmashauri ya wilaya ya Njombe ambapo vijiji vitatu bora na kijiji cha Wanginyi kikichukua nafasi ya kwanza kwa vijiji vyote Tanzania.

Emmanuel Mwenda ni Mwenyekiti wa kijiji cha Wanginyi mshindi wa kwaza kitaifa anabainisha changamoto walizopitia kuupata ushindi huo.

“Katika mashindano haya tulikumbana na changamoto ya maji na tatizo hili mpaka sasa lipo katika vijiji ninakotoka na vyoo vya masinki bila kuwapo kwa maji usafi wake ni mgumu naomba serikali kutusaidia maji yakapatikana” alisema Mwenda

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri mbali na kuwapongeza washindi kitaifa alisema changamoto ya maji kweye wilaya yake ishughurikiwe na wakirugenzi ili wananchi wafanye shughuli zao na kuachana na mahangaiko ya kutafuta maji.