WIKI YA UNYWAJI MAZIWA YAZIDULIWA NJOMBE KITAIFA IKIWA WAKATI MKOA HUO UKIWA NA ASILIMIA 52 ZA UTAPIA MLO

SERIKALI imetoa agizo kwa waguregenzi nchini kuanzisha miradi ya ufugazi wa ng’ombe ili kuwasaidia wanafunzi kupata maziwa shuleni na kuwajengea tabia ya unywaji wa maziwa wakiwa bado wadogo.

Agizo hilo limetolewa na kaimu mkuu wa mkoa wa Njombe na mkuu wa wilaya ya Ludewa, Anatory Choya, wakati akizindua wiki ya unywaji wa maziwa kitaifa ambayo inaadhimishwa mkoani Njombe kitaifa wakati kukiwa na asilimia 52 ya udumavu mkoani humo.

Alisema kuwa mkoa wa Njombe ndio unaonoza kwa  kufuga ngombe  wanaotoa maziwa kwa wingi lakini wakazi wake hawanywi maziwa.

“Mkoa wa njombe una ng'ombewa maziwa wapatao 15,412 ambao huzalisha   8,696,440 ambapo kwa wastwastania kila wana Njombe anakuywa robo lita kwa siku huu ni mwanzo  mzuri lakini ipo  ya ya kuongeza  nguvu  ya uzalishaji," alisema  Choya.

Ameongeza kuwa serikali kama itataka kila shule kuwa na maziwa halmashauri hazita weza kifedha basi zianzishe miradi ya ufugaji wa ng’ombe mashuleni.


Katika maadhimisho hayo Ofisa mifugo mkuu Wizara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi Abdallah Temba alisema selikali inasambaza madume Bora ya Ng'ombe ya Mbegu ili kuwasaidia wafugaji kupata Ng’ombe wa Mbegu kwa urahisi.


 “Serikari kwa kushirikiana na wadau inahakikisha kuwa inazalusha ng'ombe bora wa maziwahasa madume yenye historia yakutoa maziwa mengi ambayo yatamsaidia mfugaji kufuga kwa tija," alisema Temba.

Hata hivyo katika maadhimisho hayo wadau mbalimbali wa maziwa wameweka mabanda yaokatika uwanja wa maonyesho ya wiki moja ambapo kutatolea elimu juu ya ufugaji bora na wananchi kujionea bidhaa za maziwa.

Mbali na hayo, Zena Issa Ofisa Viwango wa Shirika la Viwango Nchini TBS alisema wameshiriki maadhimisho hayo ili kutoa elimu kwa  jamii ili kutumia bidhaa zilizo sindikwa na kuthibitishwa na shiriki la viwango na kuwataka wananvhi kuhakikisha wanakuwa mbali na bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.

Alisema kuwa kwa bidhaavza maziwa ambazo hazijasibitishwa zinakuwa hazina nembo ya TBS na wananchi wawe wachunguzi ili kupata vitu bora.

“Ukiona bidhaa za kampuni moja zingine zina arama ya ubora na zinine hazina basi ujuembazo hazina bado hazijakidhi viwango vya ubura," alisema Issa.

Hata hivyo afisa masoko wa TBS Debora Haule, alisema kuwa kupitia maonyesho hayo wasindikaji wanakaribishwa katika banda lao ili kujua taratibu za kuthibitisha bidhaa zao kabla hawajaziingiza sokoni




Watoto wakinywa maziwa baada ya kuzinguliwa wiki ya unywaji maziwa kitaifa mkoani