Madereva waonywa vipande vya chungwa na pipi


IMEDAIWA kuwa majambazi na wezi wa pikipiki wamekuwa wakitumia vipande vya Chungwa na Pipi kupaka madawa ya kulevya kuwalevya madereva wa pikipiki kisha Kuwaibia vyombo vyao vya usafiri.

Kutokana na kubainika kwa kuwapo kwa kuwekewa madawa ya kulevya katika zawadi hizo madereva wa Bodaboda na Bajaji wametakiwa kuepuka kupokea zawadi ndogondogo za Pipi, Chungwa na soda wawapo kazini kutoka kwa wateja wao.

Akizungumza Mkoani Njombe Mkurugezi wa taasisi inayo toa mafunzo kwa madereva hao ya Apec Respicius Timanywa alisema kuwa madereva wengi wamekuwa wakijikuta wamelewa na chombo chao kimeondoka kutokanana kupewa zawadi na wateja wao.

“Dereva jiadhali na kupokea zawadi kutoka kwa mteja wako hasa zawadi za kula jail maisha yako kwa kuwa mwangalifu na mteja kama anakupenda basi akupe pesa zaidi kuliko kukupa soda akikupa soda mwambie nimekunywa mda sio mrefu,” Alisema Timanywa.

Madereva hao wamekuli kuto zijua sheria za barabarani awali kabla ya kumaliza mafunzo hayo na kluwa sasa wamejifunza na kuwa wataondoa ajali za barabarani kutokana na elimu waliyo ipata kwa muda wa wiki moja Mkoani Njombe.

Alisema kuwa awali walikuwa hawaelewi kuwa pikipiki inatakiwa kuwashwa taa muda wote inapo kuwa barabarani na kuwa sasa watawasha taa inayo wasaidia kuonekana wawapo barabarani.

Mmoja kati ya wanawake watano walio pata mafunzo ya udereva mkoani Njombe dereva wa bajaji, Veronica Msigwa alisema kuwa walikiwa wakifanya kazi hizo bila kujua haki zao wakiwa barabarani kwa kuwa walikuwa wakiwakimbia askali wa usalama barabarani na maranyingine wakiwaonyesha reseni zao walizolipata kwa nyia ya panya bila kupata mafunzo.

“Zamani tulikuwa tunafanya kazi hii kwa uzoefu tu tulikuwa hatujapata mafunzo ya aina yoyote na trafiki wakitudai reseni tulikuwa tunawaonyesha reseni ambazo tulizipata wakati hatujapata mafunzo ya usalama barabarani lakini sasa tutakuwa tunazijua haki zetu tuwapo barabarani,” alisema Msigwa.
Kaimu kamada wa polisi mkoa wa Njombe Nicodemus  Katembo alisema kuwa madereva hao wahakikishe kuwa wanaheshimu kazi yao na kufanya kazi hiyo kwa uadhilifu kwa kuwa inawafanya kuendesha maisha yao na familia zao kuzifanya kuwa vizuri.