Madereva Bajaji, Bodaboda 300 Makambako wafuzu mafunzo



JESHI la Polisi nchini limetakiwa kutoa elimu kwa madereva pikipiki za magurudumu matatu na mawili maarufu kama  Bodaboda na Bajaji kuhusina na usalama wa barabarani kabla ya kuanza kuwakamata kwa makosa hayo kitu kitakacho saidia kupinguza ajali za Barabarani hapa nchini.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Apec, Respicius Timanywa wakati wa kufunga mafunzo kwa madereva bodaboda na Bajaji Halmashauri ya mji Makambako mkoani Njombe, ambapo madereva 300 wamefuzu mafunzo ya usalama barabarani na kuwatambua watekaji wa vyombo vyao.

Timanywa alisema kuwa haiwezekani madereva hao wakawa wanakamatwa kabla hawaja patiwa elimu ya usalama barabarani kwa kuwa wanavunja sheria hizo kwa kuto jua na kuwa baada ya kutolewa kwa mafunzo hayo jeshi la polisi mkoani Njombe linaweza kuanza kufanya msako wa madereva ambao wamekuwa hawata reseni na wasio fuata seria za usalama barabarani.


Alisema kuwa kwa elimu ambayo wamitoa madereva wahakikishe kuwa wanazingatia wanapo kuwa barabarani na kujiadhali na zawadi vya kula kutoka kwa wateja wao kwa kuwa Chungwa na pipi ni vitu vinavyo weza kuwekwa madawa ya kulevya na kusababisha kutekwa na waharifu.

Aidha aliwataka madereva hao kutoa taarifa za waharifu kwa jeshi la polisi pale wanapo ona kuna dalili za kuwapo kwa wahalifu kwa kuwa vyombo vyao vimedaiwa kuhusishwa sana na uharifu hapa nchini.

Alisema kuwa kutokana na elimu wanayoitoa katoka mikoa 20 hapa nchini madereva walio wapatia elimu hakuna hata mmoja aliye pata ajali na kuwa ajali za Pikipiki zimepungua.

Alisema kuwa mafunzo hayo yamesaidia kuwafanya madereva hao kuwa na uhusioano mzuri na Jeshi la Polisi hapa nchini na kusaidia kufichua wahalifu.
 
Akizungumzia upungufu wa ajali za barabarani zilizo kuwa zikitokana na madereva Bodaboda Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Kelvin Ndimbo alisema kuwa kwa sasa ajali zimepungua kabisa zinazotokana na madereva bodaboda.

“Mkoa wa Njombe kutokana na elimu zinazotolewa na wadau mbalimbali ajili za boda boda zimeisha kuna miezi ajali hizo hakuna kabisa hii inaonyesha kuwa ajaili zilikuwa zinatokana kutokana na madereva wazembe,” alisema Ndombo.

Mgeni rasimi katika Hafra hiyo ya kufunga mafunzo na kukabidhi vyeti kwa madereva hao Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Necodemus Katembo alisema kuwa kutokana na mafunzo waliyo pewa na shirika hilo kuna uhakika wa kupungua kwa ajali na matukio ya uharifu kwa kuwa shirika hilo mafunzo hayo yanatolewa ikiwa ni kwa mala ya pili.

“Naimani kwa sasa tumepata wakufunzi wengi nyinyi mkawe waalimu kw


a wenzenu ambao hawajafika kwenye mafunzo haya, naamini kuwa mlikuwa hamjui kuwa pikipiki zenu zinatakiwa kuwashwa taa hata mchana lakiji sasa mnalitambua hilo kawaambieni na wenzenu,” alisema Katembo.


Baadhi ya madereva wamesema kuwa walikuwa wakisababisha ajali kwa kuto jua baadhi ya sheria za barabarani na kuwa kwa sasa wanafahamu alama zote za barabarani na kuomba mamlaka inayo husika na miundombinu ya barabara kuhakikisha kuwa kunakuwepo na vibao vya alama za barabarani ili kuto wasababishia ajali.