DC awataka bodaboda kujiunga na bima za afya

MADEREVA  wa bodaboda nchini wametakiwa kukata bima ya afya ili kutibiwa watakapougua wao pamoja na wategemezi wao watano kwa kuwa ugonjwa hautoi taarifa.

wito huo umetolewana mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe, Yasina Mshama wakati akifunga mafunzo kwa madereva wa bodaboda halmashauri ya wilaya ya makambako ambao wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani pamoja na utunzaji wa pesa zao.

Alisema kuwa madereva hao wajiunga na bima za afya kubwa ili kutpata huduma katika hospitali kubwa na kupata huduma yenye uhakika kuliko wakikata bima ndogo ambazo huduma zinaishia katika zahanati.

Alisema kuwa madereva hao wakiwa na bima kubwa watatibiwa wao pamoja na familia zao mpaka watu watano kuliko wakikata bima ndogo itamtibu mtu mmoja na katika kituo cha afya cha kata yake.

Kwa upande wake mkuregenzi wa taasisi iliyo toa mafunzo kwa madereva hao 130 ya Apec Respicius Timanywa huku wanawake wakiwa ni wanne akiwemo diwani wa Kata ya Udonja alisema kuwa madereva hao ni vyema wakapata bima ya afya kwa kuwa wakiwa na bima hiyo watatibiwa wakati wowote kwa mwaka mzima bure baada ya kulipa mara moja.

Alisema kuwa wamekuwa wakipata vipato vyao kidogo lakini wakumbuke kuweka kidogokidogo kasha kulipa bima ya afya huku akiiomba serikali kuruhusu pikipiki kuwa na bima kubwa tofauti na ilivyo hivi sasa.

Timanywa Alisema kuwa halmashauri kupitia mapato yake ihakikishe kuwa inatenga asilimia 5 kwaajili ya vijana na kuwapatia vijana walio pata mafunzo ili kuwaendeleza kiuchumi na hatimaye kujitegemea.

Hata hivyo diwani wa kata ya Udonja Happiness Bomber ameomba Apec kutoa tema mafunzo ili wananchi wake wapate elimu hiyo na kupunguza ajali kwa kuwa wananchi wengi wamekuwa wakijifunza bodaboda mtaani na kuingia kusafirisha abiria.