TASOI Yazinduwa Kampeni ya Saratani kwa Kutumia Technolojia


Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo akizungumza na waandhishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia technolojia ya mawasiliano bila malipo yoyote katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo jijini Dar.
Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo akizungumza na waandhishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia technolojia ya mawasiliano bila malipo yoyote katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo jijini Dar.
Dk. Dominista Kombe ambaye ni Mshauri kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road akitoa takwimu ya wagonjwa wanaofika kutibiwa katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage  akizungumza akieleza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo.
 Waandishi wa habari wakiendelea kuchuka habari
 Mkutano ukiendelea
 
Na Michael Maurus, Dar es Salaam
ASASI isiyo ya kiserikali ya Tanzania Social Outreach Initiative (TASOI),
imezindua kampeni rasmi mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya
Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano bila malipo
yoyote.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo,
alisema kuwa kampeni hiyo itatoa elimu, uhamasishaji na kutoa ushauri nasaha
kwa wananchi kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS).
Alisema kuwa katika kampeni hiyo, TASOI inashirikiana na wadau mbalimbali
katika masuala ya afya, teknolojia na uhamasishaji wa jamii ili kutoa huduma
hii muhimu bila malipo au gharama yoyote kwa watumiaji wa simu za mikononi.
“Kwa kumnukuu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Yasiyoambukiza
Wizara ya Afya, Profesa Ayoub Mgimba, ‘Hali halisi inadhihirisha kwamba
magonjwa yasiyoambukiza kama saratani hivi sasa yamekuwa ni tatizo kubwa hasa
katika nchi kama yetu ambapo ufahamu na mwamko ni mdogo sana juu mazingira
hatarishi, viashiria, matibabu na matunzo ya wahanga wa magonjwa haya. Saratani
inasababisha madhara makubwa ambayo yanaelekea kuwa majanga kwa jamii na
kiuchumi kwa Taifa.”
Akielezea jinsi kampeni hiyo itakavyoendeshwa, Hellen alisema kuwa kwa
muda wa miezi sita, watumiaji wa simu za mkononi za mitandao yote nchini,
wataweza kupata taarifa za saratani kwa kupitia namba 15774 kwa kutuma neno
CANCER au SARATANI kwenda namba hiyo na kuchagua lugha anayotaka kupokea
taarifa hiyo, iwe ni Kiswahili au Kiingeza.
“Hapo utapokea ujumbe wenye elimu juu ya saratani, kati ya za viungo vya
uzazi, yaani tezi dume, saratani ya matiti na shinga ya kizazi. Huduma hii
itapatikana kupitia mitandao yote ya simu nchini, Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel
na TTCL,” alisema.
Aliongeza: “Tungependa pia kuwashirikisha wananchi wote kuchangia kwa
hiyari ili tutimize malengo haya kwa pamoja. Na hii unaweza kuchangia Sh 1200
kwa mwezi au Sh 300 kwa wiki.
“Hili utaweza kulifanya kwa kukubali kupokea ujumbe mfupi kutoka kwetu
ambao utakuwa na gharama ndogo ya Sh 150 tu. Pia unaweza kuchangia kupitia
ezypesa, m-pesa, tigopesa, airtel money. Uchangiaji huu ni wa hiyari na hauzuii
kupata huduma ya elimu ya saratani.”
Kwa upande wake, Daktari bingwa wa kwanza wa saratani mwanamke Tanzania, Dominista
Kombe wa Ocean Road Cancer Istitute, alisema kuwa ni kweli saratani ni janga la
jamii, hali halisi hapa Tanzania, saratani ni tatizo kubwa na linaongezeka kwa
kasi, ni jumla ya ugonjwa wa HIV na ugonjwa wa TB, tatizo la saratani
lilitakiwa kupewa kipaumbele zaidi.
“Tatizo jamii huwa haipo tayari kuweka wazi juu ya uginjwa huu kwa
kuogopa aibu ya kutengwa, haya yote yakitokana na uhafamu mdogo juu ya ugonjwa
huu,” alisema.
Alisema kuwa serikali imekuwa ikijitahidi kupambana na ugonjwa huu kwa
kutoa huduma bure, lakini hata hivyo imejikuta ikishindwa katika kukabiliana
nalo kwani tatizo ni kubwa mno, akiitaka jamii kusaidia katika vita hiyo kama
walivyoamua kufanya TASOI waliokuja na mpango wao wa kampeni kupitia simu
kuiwezesha jamii kujua juu ya viashiria vya janga hilo.
Alisema kuwa tatizo la saratani ni la dunia nzima, hivyo kuna ulazima wa
jamii kujenga utaratibu wa kupima afya mara kwa mara kama ilivyo kwa nchi za
Ulaya ambako imesaidia kupunguza ukubwa wa janga hilo kupitia chanjo.
Alisema kuwa Ocean Road hupokea wagongwa wapya 5000 kwa mwaka, kati yao
asilimia 80, wanafika wakiwa katika hali mbaya kiasi kwamba hupewa tiba ya
kuwaongezea siku tu, huku asilimia ndogo sana, huwahi na kupewa tiba
inayowawezesha kuishi.

By ThehabariBlog