TAMKO KUTOKA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NCHINI NA VIDEO KIFO CHA MCHUNGAJI MTIKILA



Kufwatia kifo cha mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati wa siasa za Tanzania ,Mwenyekiti wa chama cha DP mchungaji Cristopher Mtikila kilichotokea juzi kwa ajali ya Gari,baraza la vyama vya siasa nchini wametangaza kuahirishwa kwa kikao cha baraza kuu la vyama vya siasa nchini kilichokuwa kifanyike tarehe 6 na 7 mwezi wa kumi visiwani Zanzibar hadi  tarehe itakayopangwa tena baada ya maziko ya marehemu mchungaji MTIKILA.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam leo Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania PETER KUGA MZIRAY amesema kuwa kamati ya uongozi ya baraza la vyama vya siasa kwa niaba ya baraza hilo wameshtushwa sana na kifo cha mwanasiasa huyo na wamekutana kwa dharura na kuamua kusogeza mbele kikao hicho ambacho kinatajwa kujadili mambo muhimu na nyeti kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

“Kifo cha mchungaji MTIKILA ni pengo kubwa sana katika siasa na democrasia ya vyama vingi nchini kwani amekuwa mdau mkubwa katika kudumisha na kuboresha mfumo wa siasa za nchi yetu na democrasia ya vyama vingi hapa nchini”amesema mziray.

Aidha baraza hilo limetoa salamu za rambi rambi na pole nyingi kwa wanafamilia ya marehemu wanachamawa DEMPCRATIC PARTY (DP) na ndugu na jamaa wote,na kuwataka wawe na moyo wa uvumilivu kwani kila mtu anaondoka duniani kwa namna na siku yake.
Mchungaji mtikila alifariki siku ya jumapili alfajiri katika ajali ya gari iliyoacha njia na kupinduka mkoani pwani wakati akiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam