Nimonia yadaiwa kumaliza watoto chini ya miaka 5

Dr. Rukia Ally
SERIKALI inaendelea kupambana na magonjwa ya kuhara na Nimonia kwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano kwa kutumia dawa zilizoboreshwa N a kufungashwa pamoja zinazoitwa ZIORA  zenye zink , ORS na amoxiline kwa ufadhili wa shirika linalo  hudumia watoto Duniani Unicef.

Tafiti zinaonyesha kuwa idadi  Kubwa ya watoto chini ya miaka mitano wanakufa kutokana na magonjwa haya ya Vichomi na kuhara ambayo kutokana na walezi kuchelewa kuwafikisha sehemu za tiba  na kuifanya  wizara ya afya kuinuka maofisini na kuelekea mikoani kufanya utafiti tangu mwaka 2013.

Baada ya uzinduzi wa Matumizi ya dawa mpya ya Ziora katika kuendeleza  mapambano dhidi ya magojwa hayo ya kuhara na vichomi kwa watoto chini ya miaka mitano kitaifa jijini Dar es salaam uliojumhisha waganga wakuu nchini watalam wa afya.

Wataalamu juzi wataalamu wamefika mkoani Njombe na kutoa mafunzo ya uhamasishaji kwa watoa huduma za afya ngazi ya mkoa na wilaya na kujumuisha viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na wakurugenzi.

Docta Rukia Ally (Pichani) ni mtaalamu wa afya kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii alieleza lengo la mafunzo hayo na kwamba yatakuwa endelevu katika mikoa  mingine Hapa nchini ndani ya miaka miwili ili kudhibidi vifo vya watoto.


“Walsha hii inalenga kutoa hamasa ya kuhakikisha watoa hudyuma za afya wanatoa huduma sahihi za afya kwa watoto na kuhakikisha vifo vitokanavyo na magonjwa haya vina koma,” alisema Dr. Ally


Washiriki wa mafunzo ya  mapambano ya magojwa hayo wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wataalamu wa afya kutoka wilaya za Njombe na Makete, mkoani Njombe wametoa ushauri kwa wizara kupeleka dawa mapema katika Hospitali, Vituo vya afya na Zahanati pamoja na kubainisha gharama za mauzo ili ziwafikie walengwa mapema na kubaisha changamoto katika utoaji wa huduma za afya maeneo yao ya kazi kama anvyoeleza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya makete Fransis Maumbo


Naye Katibu tawala mkoa wa Njombe Jackison Saitabau, wakati wakifungua na kufunga mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku moja pamoja na kuwapongeza Unicef na  kwa ufadhili mkubwa wanaotoa kwenye sekta ya afya amewataka washiriki kutekeleza kwa vitendo elimu walioipata pamoja na kifikisha kwa watumishi wengine wa afya na wazazi