Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Mkamba akizungumza na wadau wa maliasili pamoja na waandishi wa habari ,ambapo alisisitiza kulinda misitu kwani uvunaji umekuwa mkubwa nahivyo kupelekea ukame katika nchi yetu pia alisisitiza kutoa elimu kwa jamii inayozungukwa na misitu hiyo katika uzinduzi wa kampeni ya mfululizo wa vipindi vipya vya runinga pamoja na uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali za hapa nchini Tanzania
Msaidizi wa Balozi, Ubalozi wa Ufini(Finland) ambao ni wafadhili wa Mama Misitu, Simo-Pekka Parviainen akizungumza jambo katika uzinduzi wa kampeni ya mfululizo wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini
Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila akiwasisitiza waandishi wa habari kutumia nafasi hiyo kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii na hata kufikisha ujumbe ulio sahihi kwa jamii.
Mkurugenzi Mtendaji Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Rahima Njaidi akitoa somo kwa wadau wa maliasili hasa katika uvunaji wa misitu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mfululizo wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini
Mkuu wa Mradi ya Kilimo, Kipato na Ajira wa Shirika la Maendeleo la Uswisi, Ueli Mauderli akitoa neno katika uzunduzi wa Kampeni ya kipindi cha Tv
Mshauri wa Ufundi Wizara ya Maliasili na Utalii, Thomas Sellaine akizungumza jambo katika uzinduzi wa kampeni ya mfululizo wa vipindi vipya vya runinga vinavyo kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitakavyo kuwa vikirushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini
Balozi wa Mama Misitu, Asha Salimu (kushoto), akizungumza jambo katika uzinduzi huo.
Meneja Kampeni Mama Misitu, Gwamaka Mwakyanjala, akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwezeshaji, Faustine Ninga(wa kwanza kulia) kutoka Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF) akizungumza jambo
Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Mkamba ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akibonyeza kwenye kopyuta mpakato kudhihirisha ufunguzi rasmi wa kampeni ya mfululizo wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa, ambavyo vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini
Wadau wa mazingira pamoja na waandishi wa habari wakiwa katika mkutano
Picha ya Pamoja
MFULULIZO wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini. Kampeni ya Mama Misitu (MMC), inazindua mfululizo wa vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu uzalishaji na faida za mkaa endelevu kijamii, kimazingira na kiuchumi.
Vipindi hivyo mfululizo vimetengenezwa katika wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya jitihada za pamoja kati ya Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Shirika la Kuendeleza Teknolojia za Asili (TATEDO) na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili kuleta mabadiliko na kurasimisha sekta ya mkaa iweze kutoa ajira endelevu na kipato kwa jamii za vijijini na mijini.
Inakadiriwa kuwa mkaa na biashara za kuni huzalisha takriban (dola bilioni 1) za mapato kwa zaidi ya wazalishaji, wasafirishaji na wafanyabiashara laki tatu (300,000) katika mwaka 2012. Mahitaji ya mkaa nchini Tanzania yameongezeka kwa kasi na kwa kiasi kikubwa.
Mkaa endelevu ni mkaa unaozalishwa kwa njia endelevu kutoka katika Misitu ya Hifadhi ya Jamii bila kuchangia ukataji miti na uharibifu wa mazingira. Hata hivyo, uzalishaji wa aina hii ya mkaa bado haujajulikana. Kampeni hii mpya ina lengo la kuleta mabadiliko kupitia ubunifu wa vipindi mfululizo vya runinga ambavyo vinazinduliwa leo.
Nishati zitokanazo na tongamotaka (biomas) ni nishati muhimu sana nchini Tanzania itakayoendelea kutumika angalau zaidi ya miaka 20 ijayo. Kwa sasa, mkaa mwingi huzalishwa kinyume na utaratibu kutoka katika misitu ya hifadhi na misitu ya vijiji isiyo na mipango ya matumizi endelevu. Kutokana na usimamizi hafifu wa uzalishaji wa mkaa, imesababisha ukataji miti na uharibifu wa misitu kuongezeka nchini Tanzania.
Kampeni ya Mama Misitu na washirika wake (TFCG na MJUMITA) inalenga kuleta mabadiliko katika sekta ya mkaa kutoka tatizo kuwa fursa kubwa muhimu. Hivyo, vipindi vya runinga vya Mama Misitu pamoja na jumbe muhimu za mawasiliano zitasambazwa nchini Tanzania ili kuibua mjadala wa pamoja juu ya kuboresha utawala bora wa rasilimali misitu na kuleta faida kwa watanzania.
Mama Misitu ni kampeni ya mawasiliano yenye lengo la kuboresha utawala bora wa misitu ya Tanzania na kupunguza uvunaji haramu wa mazao ya misitu ili watu wa Tanzania wanufaike zaidi na rasilimali misitu zao.