Tottenham cha Bao 4-1.Man City

Harry Kane akishamngilia bao lake la kwanza kwa msimu huu dhidi ya Manchester City 

VINARA wa Ligi Kuu ya Ungereza Manchester City leo wamekumbwa na kizaza zaa baada ya kukubali kichapo kutoka kwa Tottenham cha Bao 4-1.

 
Man City ndio walikuwa wakwanza kupata goli katika dakika ya 25 kupitia Kevin De Bruyne kabla ya Eric Dier wa Spurs kusawazisha golihilo na kutoa mwanya kwa nyongeza ya magoli mengine matatu katika mchezo huo. 

Toby Alderweireld  aliinandikia goli la pili Spurs kasha Harry Kane kufunga bao la tatu lililotokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Christian Eriksen na Erik La,ela alifunga pazia la karamu ya magoli kwa Spurs kwa kupachia bao la 4 katika dakika ya 79 na kufanya matokeo ya mchezo huo kumalizika kwa 4-1.



Alderwereld (kati) akiruka kichwa nakupiga mpira uliomshinda mlinda mlango Caballero.



Dier akipongezwa na wachezaji wenzake wa Spurs Dele Alli (kulia) baada ya kuisawazishia timu yake na kufanya matokeo 1-1.



Kiungo wa Tottenham raia wa Denmark Christian Eriksen akibanwa mbavu na wachezaji wa Man City. Kulia ni Bacary Sagna.