Mama Fatma Karume Azindua Michuano ya Mpira wa Mikono Karume Cup Uwanja wa Gymkhana Zanzibar


Mlezi wa Michuano ya Kombe la Karume Cup Mama Shadya Karume akiwa na Viongozi wa Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar (BAZA) akiwasili katika viwanja vya Gymkhana kwa ajili ya ufunguzi wa Michuano hiyo ya 12 ya Karume Cup tangu kuazisha. 
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mareheme Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume akisalimiana na Viongozi wa Michezo Zanzibar wakati akiwasili katika viwanja vya Gymkhana kwa ajili ya kufungua Michuano ya 12 ya Karume Cup kwa mchezo wa Basketi Ball, akiwa mgeni rasmin wa michuano hiyo inayoshirikisha timu 17 za Wanawake  inashirikisha timu 6 na Wanaume inashirikisha timu 11.
Mama Fatma Karume akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi Sharifa Khamis (Shery) wakati akiwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya ufunguzi wa michuano ya Karume Cup kwa mchezo wa Basketi Ball.
Mama Fatma Karume akisalimiana na Mjuu wake Ahmeid Abeid Karume wakati akiwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya ufunguzi wa michuano hiyo.
Washiriki wa Michuano ya Karume Cup wakiingia uwanjani kwa maandamano kwa ajili ya Ufunguzi wa Michuano ya Mpira wa Mikono (Basketi Ball) uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar  
Washiriki wa Michuano ya Karume Cup wakiingia uwanjani kwa maandamano kwa ajili ya Ufunguzi wa Michuano ya Mpira wa Mikono (Basketi Ball) uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar 




 

Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume akizundua michuano ya Mpira wa Mikono (Basket Ball) Kombe la Karume Cup katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar, akirusha mpira kufunga basketi wakati wa uzinduzi huo.