
Gavana katika eneo la Mecca ameamrisha kufanyika uchunguzi kufuatia kuanguka kwa kreni katika msikiti mkubwa zaidi duniani.

Utawala nchini Saudi Arabia unasema kuwa upepo mkali ndio ulisababisha kreni iliyokuwa ikitumika kwa ujenzi kuanguka kwa msikiti mkubwa mjini mecca ambapo watu 107 waliuawa na wengine takriban 200 kujeruhiwa.

Mkuu wa idara ya ulinzi wa angani nchini humo alisema kuwa kulikuwa na mvua kubwa wakati ajali hiyo ilipotokea na upepo ulikuwa ukivuma kwa takriban kilomita 83 kwa saa.

Msikiti huo unazunguka eneo takatifu la kiislamu la Kaaba na ndio msikiti mkubwa zaidi duniani na huwavutia mamia ya waislamu ambao huenda kuhiji kila mwaka.


CHANZO: BBC SWAHILI