Kiwanda cha chai cha Lupembe Mwezi Disemba kitaanza kushugulikiwa na kuanza kufanya kazi



Mohamed Mnyaa akizungumza na wakazi wa jimbo la Lupembe mkoani Njombe katika kampeni za uchaguzi za ukawa Mgombea mwenza wa Ukawa Juma Haji Duni jana 
Mzee wa kijiji cha Lupembe, David Lupembe akitoa dukuduku lake juu ya Chama cha Mapiduzi kilivyo funga kiwanda kwa muda wa miaka 6 huku vijana wao wakikosa ajila 

Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar Said Issa Mohamed akimkaribisha Mgombea mwenza wa umoja wa Ukawa Juma Haji Duni, katika mkutano wa kampeni katika jimbo la Lupembe mkoani Njombe 

Wananchi wa kijiji cha Lupembe wakisikiliza kwamakini sera za ukawa huku wakipewa matumaini ya kufunguliwa kiwanda cha chai kwa maslahi yao.
Watoto nao wapo makini kusikiliza sera za Ukawa
Mgombea mwenza wa Uraisi wa Ukawa Juma Duni akizungumza na wakazi wa jimbo la Lupembe mkoani Njombe katika moja ya mikutano ya kampeni na akimuonyeshea mfano mtoto ambaye anatakiwa kupata haki yake ya elimu. 
Mgombea Mwenza wa Ukawa Juma Duni akimnadi mgombea wa Ubunge jimbo la Lupembe,Edwin Swale na kuomba kura za wakazi hao wa Diwani wa kata za jimbo hilo kura za Jimbo hilo la Lipembe lenye changamoto kubwa ya kukosa kiwanda huku wananchi wakikitegemea kiwanda hicho kutokana na kuwa ni wakulima wa chai.
Mgombea Ubunge Edwin Swale akijinadi kwa wananchi wa Lupembe pembeni Mgombea mwenza Wa Ukawa Juma Duni
Wananchi wakimsikiliza mgombea Ubunge wao





UMOJA wa katiba ya wananchi Ukawa wamesema kuwa wakiingia madarakani wataanza kushugulikia kiwanda cha chai cha Ivyulu, Lupembe ambacho kimefungwa kutokana na mgomo wa wananchi kuchuma chai na kuwapo kwa kesi mahakamani.


Hayo yamebainishwa na Mgombea mwenza wa urais Chadema, chini ya Ukawa Juma Duni akiwa katika kampeni za uchaguzi katika jimbo la Lupembe mkoani Njombe ambapo wananchi waliulizwa juu wa kelo walizonazo katika jimbo hilo.


Duni alisema kuwa wananchi wa Lupembe wakiwachagua ukawa mwezi disemba mwaka huu kiwanda hicho kitaanza kushughulikiwa na kuanza kufanya kazi na vijana wa eneo hilo kuanza kupata ajila katika kiwanda cha nyumbani huku wazaziwao kuanza kuingiza fedha kutokana na uuzaji wa chai.

Alisema wakichagua Ukawa na kuwapelekea mgombea ubunge wa Ukawa, anaye gombea kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, Edwin Swale na madewani wake alisema kuwa mbunge wao apeleke matatizo yao ya kiwanda na mendine ili yaanze kushughulikiwa na kuanza kunufaika na kiwanda hichio.

 "Wananchi wa Lupembe kufikia mwezi Disema mara baada ya uchaguzi mbunge wenu atakija Ikulu na kutuambia matatizo ya kiwanda chenu nini kilisababishwa kifungwe na tutaanza kushughulikia mapema na kuanza kunufaika na kiwanda hiki," alisema Duni.

Aliongeza kuwa kiwanda hicho kitachunguzwa chanzo cha kufungwa na kuanza kufanya kazi ili kuinua maisha ya wana Lupembe na wakazi wa mkoa wa njombe kwa ujumla wanao lima chai.

Awali wananchi walipo pewa nafasi ya kuyasema matatizo yanayo wakabili mmoja wa wananchi Magreth Kabelege alisema kuwa katika jimbo hilo wanakabiliwa na changamoto ya kufungiwa kiwanda chao ambacho walikuwa wakikitegemea kwa kuingiza kipato chao cha kila siku.


"Kwa kweli kiwanda hiki wakazi wa jimbo la Lupembe tulikuwa tunategemea lakini kimefungwa baada ya kuona sisi tunauza chai kwa bei ya chini ya shilingi 250 na wenzetu wa Wilayani Rungwe mkoani Mbeya wakiuza chai kwa shilingi 500, tunaomba mtusaidie kwa hilo wananchi wa lupembe maana tuliona tunakandamizwa," alisema Kabelege.


Mgombea wa Ubunge Edwin Swale alisema kuwa akipewa kura za kutosha na wananchi wa jimbo hilo atahakikisha kuwa wananchi wanapata kiwanda hicho kwa kupeleka kwa ngazi ya juu ili kishughulikiwe na kuanza kuingiza kipato chao na kufanya maisha kuwa rahisi na vijana kuw ana ajira.


Alisema kuwa wananchi wampe kura za kutosha katika ili kuweza kuingia bungeni na kutetea maslahi ya jimbo lake na kuhu akisema kuwa wananchi wa jimbo hilo wanatarajiwa kuingizwa katika mtego wa deni kubwa na moja ya kiwanda ambacho kinatarajiwa kuanzishwa katika maeneo yao.

Alisema kwua wananchi hao wanatarajia kusainishwa mkataba na kiwanda cha chai ambacho wananchi watakopeshwa hisa na baadae wataanza kudaiwa pesa nyingi ambazo zitakuwa ni mzigo.


"Wananchi katika kiwanda cha zamani kilikuwa cha wananchi lakini kiliuzwa na kesi walishindwa wanadaiwa bilioni 1 na gharama zingine za kesi na kuna kiwanda kipya kinacho anzishwa wananchi wanatakiwa kuwa na hisa asilimia 25 na hisa hizo wanakopeshwa wakikopa hisa hizo watakiwa wanadaiwa bilioni 3 na zaidi" alisema Swale.