Kata ya Igurusi yapata mwanamke mzoefu mgombea udiwani CCM

MGOMBEA udiwani kata ya Igurusi na aliyekuwa diwani wa viti maalumu halmashauri ya Mbarali Mkoani  Mbeya Hawa Kihwele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameiomba serikali kutoa elimu ya uraia kwa wapiga kura wake ili kuwa na elimu ya mpiga kura na kuelewa maana ya uhuru wa kuchagua na kucaguliwa.

Akizungumza na kituo hIki Kihwele amesema kuwa katika kata yake kumekuwa na watu ambao elimu ya uraia haija wafikia ambapo wanafikia hatua ya kuto heshimu haki ya mtu kugombea katika nafasi ya kisiasa.

Alisema kuwa anashukuru serikali kuendelea kutoa elimu hiyo katika shule za kata licha elimu hiyo kuwafikia walioko shuleni pekee.

"Kwa sasa baadhi ya wananchi wanaelewa kuhusu siasa ambapo wanapata mashuleni katika shule zilizopo katika kata hii lakini hawapeleki kwa wenzao ambao hawaja badatika kwenda shule," alisema Kihwele.

Alisema kwua elimu ya siasa inayo tolewa shuleni na kwa wanao jifunza kutoka katika vyombo vya habari vingine wananchi wanao bahatika kuipata waifikishe kwa wenzao ambao haijawafikia.

Aliongeza kuwa amesukumwa kugombea kata hiyo kutokana na kuisha katika kata hiyo kwa zaidi ya miaka 15 huku akielewa matatizo ya wakazi wa kata hoyo na kuahidi kuyatatua kwa kusimamia kidete kodi zao akiwa katika baraza la madiwani wa halmashauri ya Mbarali.

"Nilikuwa katika Bara la Madiwani kwa miaka mitano sasa nataka kuingia kama diwani ili nitekeleze yale niliyoona wananchi wanayahitaji kwa kata hii ya Igurusi," aloongeza Kihwele.

Hata hivyo aliwaomba wakazi wa kata ya Igurusi kumchagua ifikapo Okopa 25 na kuwa pia kuwachaguwa viongozi wa juu yake Dr John Magufuri na mbunge wa jimbo la Mabari Haroon PirMohamed .