Emirates yamtambulisha Meneja mpya wa Tanzania


*Ni Bw. Husain Alsafi
Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipokuwa akijitambulisha, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akizungumza na waandishi wa habari (kushoto), wakati alipokuwa akijitambulisha, Dar es Salaam jana.  
Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akijitambulisha, Dar es Salaam jana.  
Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, alipozungumza nao, kuhusu mafanikio na matarajio ya shirika, wakati akijitambulisha, Dar es Salaam jana. 

Na Mwandishi wetu
SHIRIKA la Ndege la Kimataifa Emirates lenye makao yake makuu Dubai, jana lilimtangaza Meneja wake mpya wa Tanzania Bw. Husain Alsafi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafLa fupi ya utambulisho wake Mtendaji huyo mpya wa Emirates Bw. Husain Alsafi alisema kwamba, Emirates imefanikiwa kufikia wastani wa asilimia 12% wa idadi ya wateja wake wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mtendaji huyo mkuu aliongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa Shirika hilo la Ndege la kimataifa linatimiza matakwa ya abiria wake hasa kwa soko la Tanzania na kwingineko, hivyo basi wameahakikisha kuwa na safari za kila siku kutoka Tanzania kwenda nchi za nje kupitia Dubai, hivyo watanzania wengi wananufaika pale wanapotumia kusafiri na shirika hilo ambapo pia wanapata faida Zaidi endapo watapanga safari zao mapema ili kupata punguzo la bei/nafuu Zaidi.