15 WANUSULIKA KIFOFO

WATU 15 wamenusulika katika ajali ya gari iliyo husisha magari mawili moja likitokea Jijini Dar kuelekea songea likiuwa na abirana na gari ya mizigo Mkoani Njombe juzi majira ya saa 1: 00 jioni.

Ajali hiyo iliyo tokea juzi Mkoani Njombe barabara ya Njombe Songea imetokea maeneo ya Yakobi imesababisha watu 15 kujeruhiwa baada ya gali waliyo kuwa wakisaria kugongana na roli la makaa ya mawe lilikokuwa limeharibika.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi wa basi na kuharibika kwa gari ya mizigo iliyo kuwa ikitokea Mkoani songea.

Akisimulia tukio hilo mtafungwa alisema kuwa gari mali ya kampuni ya New Force iliyo kuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam ili msinda dereva na kugonga gari ya makaa ya mawe iliyo kuwa imeharibika katika mteremko wa Yakobi.

Alisema kuwa licha ya dereva wa basi la abilia kushindwa kulimudu basi hilo roli la makaa ya mawe lililokuwa limeharibika lilishindwa kuweka alama za barabarani kuonyesha kuwa limeharibika.

Akielezea ajali hiyo ilivyo tokea dereva wa basi ya New Force Godfrey Mahenge alisema kuwa alishindwa kuona gari hiyo iliyo haribika ka kuwa haikuwa na alama yoyote iliyo kuwa ikionyesha  kunagari iliyo haribika.

Alisema kuwa gari hiyo iliyo kuwa imeharibika haikuwa hata na mikanda inayo ngaa ambayo ingeonyesha kuwa kuna gari kiasi kuwamba aliliona gari kwa Ghafla na kushindwa kulikwepa.

Aidha kwa upande wao baadhi ya abilia walio jeruhiwa na kurazwa katika Hospitali ya Kibena Mkoani Njombe walisema kuwa wamenusulika na kifi kutokan ana kuwa walikuwa wamevaa mikanda, na kuwa baada ya kutokea ajali hiyo walianza kutokea maderishani.

Watu walio lazwa katika hospitari hiyo wengi wao wanamajeraha madogo na wanaweza kuruhusiwa wakati wowote huku baadhi yao wakiwa wamevungika miguu.

Mwisho
Picha Kmanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad mtafungwa akizungumza na waandishi wa habari katika endeo la ajali ya Basi la New force  iliyo tokea juzi mkoaninjombe