WAUMINI mbalimbali hapa nchini wametakiwa kutumia vizuri
kipindi hiki cha uchaguzi kwani wakifanya vibaya sasa watapata shida miaka
mitano, na kuepuka wanao wapa pesa na kuonywa kuwa hizo sio pesa ni rushwa.
Wito huo umetolewa na mchungaji wa kanisa la Pendekosti
Holiness Mission la mkoa wa Njombe Mch. Joseph Mtweve akiwa katiba ibada ya
Jumapili iliyopita.
Alisema kuwa katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe viongozi
wa dini na madhehebu mbalimbali wameenda timu ya kuliombea taifa dhidi ya
machafuko na viashiria mabilmbali vya machafuko na upotevu wa amani.
Alisema kuwa waumini na Watanzania kwa ujumla mwaka huu
wanatakiwa kuhakikisha wanaepuka kupewa poesa na watu wanao gombea kwa kuwa
wanawapa pesa na misaada hiyo sio misaada ni Rushwa kwa kuwa kipindi chote mtu
huyo hakuona umuhimu wa kusaidia jamii lakini kipindi cha uchaguzi ndio wanaona
ndio mwafaka wa kutoa misaada.
Alisema kuwa: “Waumini kipindi hiki tulicho nacho ni kigumu
kufanya maamuzi ya miaka mitano ijayo kama tukifanya vizuri kipindi hiki basi
kwa miaka mitano tutakiwa vizuri na tukifanya vibaya ni kwa miaka mitano ndio
tutaondoa ubaya huu,” alisema Mtweve.
Alisema kuwa haiwezekani kwa mkristo kuwa na makundi wakati
huu mkristo kazi yake ni kuombea ili Mungu atoe kiongozi bora kama wakristo
wakiwa na makundi hapo watachagua kiongozi kwa utashi wao.
Wakati huo huo amewataka waumini kote nchini kuhakikisha
kuwa wanaenda kupiga kura siku ya kupiga kura kwa kuwa bila kufanya hivyo
watachaguliwa kiongozi wasiye mtaka.
“Siku ya uchaguzi wote wenyesifa mkapige kura haitawezekana
kuwaachia watu wengine wakawapigia kura mkachague kiongozi ambaye anafaa na
hatoi toi rushwa ili kuwa na kiongozi anayefaa,” alisema Mtweve.
Alisema wakati kumebakiwa na miezi michache kumekuwa na
ushawishi badili kwa wanao wania uongozi wananchi wajiepushe nao hao hawana
dhamira ya kweli ya kuongeza wananchi.
Alisema kuwa ukiona mtu anatoa pesa huyo anaenda kuchukua
uongozi kwa manufaa yake mwenyewe ndio maana anaingia gharama za kutoa pesa ili
apate.