WANANCHI wametakiwa kuwa natulivu na kuto shusha bendera za
vyama wanavyo vichukia ili kuepusha migongano na vurugu wakati wa kipindi hiki
cha uchaguzi.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihanga,
Cristofa Ng’olo, wakati wa Uzinduzi wa kampeni za Chama cha Act Wazalendo,
ambacho kimemsimamisha Elimian Msigwa kugombea jimbo la Njombe Kusini, alisema
kuwa wananchi wanatakiwa kuwa watulivu wakati huu wa uchaguzi.
Katika uzinduzi huo am,bao jeshi la polisi halikuwapo ili
kuimalisha ulinzi inadaiwa kuwa kabla ya kufanyika kwa mkutano kulikuwepo kwa
hatiati ya kufanyika vurugu kutokana na baadhi ya wananchi kutaka kushusha
bendera za Chadema ambazo zimetawara kila kona za kijiji hicho.
Ng’olo alisema kuwa wananchi hawapaswi kushusha bendera za
chama chochote bila ya makubaliano na wanachama wa chama husika kwa kuwa kwa
kufanya hivyo wanaweza kusababisha vurugu.
Aidha kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji na kaim afisa
mtendaji wa kata hiyo Aderehad Mlowe alisema kuwa juzi majira ya mchana
kulitaka kutokea vurugu baada ya
wananchama wa chama Cha ACT Wazarendo kutaka kushusha bendera za chama cha
Chadema.
Alisema kuwa alitoa elimu kwa wanachama ili wasifanye hivyo
bila ruhusa ya wenyechama husika.
Aidha kwa upande wake mgombea hiyo ambaye alikuwa ni mtiania
wa Chadema Emilian Msigwa alisema kuwa ACT haina ubaya na chama chochote cha
siasa na kuwa wananchi wanatakiwa kuangalia ni nani anawafaa ili kumchagua.
Alisema kuwa ameamua kuingiza huko ili kutetea maslahi ya
wananchi na kuwa wananchi wamchague bili kuangalia chama alichonacho kwa kuwa
sera za chama ndilo zitakazo waletea wananchi usawa na haki.
Alisema kuwa mtu wanatakiwa kusikiliza sera za wagombea na
mwisho wa siku kumpigia kura bira kujali katika eneo lao kuna bendera za chama
kwa kuwa siku ya uchaguzi bendera zote za vyama zitashushwa.