WAGOMBEA ubunge waliopita katika kura za maoni
wilaya ya Njombe yenye majimbo matatu, kupitia chama cha mapinduzi CCM wamesema
kuwa baada ya kufunguliwa kwa mampeni mpaka uchaguzi wataingia kusinda na sio
kushindana.
Wakizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo
wagombea hao walisema kuwa vyama vya upinzani vitakuwa na mbio fupi kwa kuwa
wanaimani na kazi zilizofanywa na chama hicho na wananchi wanaimani nao.
Edward Mwalongo mgombea wa ubunge aliyepita
katika kura za maoni katika jimbo la Njombe kusini lililokuwa chini ya Spika wa
bunge Anna Makinda alisema kuwa jina likirudi kupelerusha bendera ya chama
hicho wapinzani mbio zao zitakuwa fupi kwa kuwa hakuna walichoi kifanya na
chama chake kuana mambio ya maendeleo kimefanya.
Alisema kuwa uchaguzi huu utakuwa rahisi kwa kuwa
mambo yaliyo fanywa yanaonekana wazi na kuwa watashinda kwa kishindo na kuwa
chama hicho kina watu wengi tofauti na wanavyo fikili wapinzani.
Aidha aliwaomba wanaCCM kuweka mshikamano wakati
wa kampeni na uchaguzi na kuunganisha nguvu kutoka kwa wagombea wote
walioshiriki katika kura za maoni ili kutoliachia jimbo hilo kwenda kwa
wapinzani.
Kwa upande wake mbunge anaye tetea kiti chake wa
jimbo la Makambako Deo Sanga alisema kuwa anawashukuru wana CCM walio mpigia
kura katika jimbo lake na kuwa anawaahidi wanachama hao na wanaMakambako wote
akiingia tena bungeni atahakikisha kuwa anakamilisha mipango aliyo kuwa
ameianza akiwa mbunge.
Alisema kuwa wapinzani wajiandae kushindwa na sio
kushinda kwa kuwa katika jimbo hilo maendeleo yanaonekana wazi wazi.
Naye mgombea wa jimbo jipya la Lupembe, Joram
Hongoli alisema kuwa anashurukuru kwa imani waliyo mpa wananchi wa jimbo hilo
jipya kwa kumteuwa katika kura za maoni na kuwa anawaahidi kutekeleza ilani ya
chama hicho na kuwa wapinzani wajipange kwelikweli kwa kuwa atatemba katika
maendeleo yaliyo fanywa na mtangulizi wake Sanga ambaye kwa sasa yupo katika
jimbo la Makambako ambalo awali lilikuwa moja mpaka jimbo lake na liliitwa
njombo la Njombe Kaskazini.