Polisi nchini Kenya wamewalaumu viongozi watatu wa kiislamu kwa kuwashawishi vijana wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu kujiunga na kundi la kiislamu la al-Shabab.
Polisi wanadai kuwa viongozi hao wa kiislamu walivuka mpaka na kuingia nchini Somalia yalipo makao makuu ya al Shabab ambapo huwashawishi vijana hao kupitia kwa mitandao.

Polisi wanadai kuwa viongozi huwahidi watu pesa nyingi ikiwa watajiunga na kundi hilo lenye mahusiano na mtandao wa al-Qaeda.
Vingozi hao hata hivyo hawajatamka lolote kufuatia madai hayo.