TANGAZO KWA UMMA. AJIRA POLISI SOMA KWA MAKINI KISHA BOFYA LINKI MWISHONI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
 


RPC.                                                                                              Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                                 Mkoa  wa  Mbeya,                                                                                    
Namba ya simu 2502572                                                                                             S. L. P. 260,
Fax - +255252503734                                                                                                      MBEYA.             
               tanpol.mbeya@gmail.com
                

JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAJULISHA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014, KIDATO CHA NNE MWAKA 2014 NA JKT MWAKA 2015 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI KUWA WANATAKIWA KURIPOTI KWA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA TAREHE 28/08/2015 KWA AJILI YA MAANDALIZI YA USAFIRI WA KWENDA SHULE YA POLISI TANZANIA
TAREHE 29/08/2015.

KILA MMOJA ATATAKIWA KUWA NA NAULI YA KUMWEZESHA KUSAFIRI TOKA MAKAO MAKUU YA MKOA ANAKOANZIA KUSAFIRI HADI SHULE YA POLISI MOSHI NA ATAREJESHEWA NAULI ATAKAPOFIKA CHUONI BAADA YA KUWASILISHA TIKETI YA SAFARI. AIDHA TAREHE YA MWISHO YA KURIPOTI CHUONI NI TAREHE 05/09/2015 NA ATAKAYERIPOTI BAADA YA HAPO HATAPOKELEWA.

AIDHA VIJANA HAO WATALAZIMIKA KUFIKA SHULENI WAKIWA NA VITU VIFUATAVYO :
1.VYETI VYAO VYOTE VYA MASOMO (ORIGINAL ACADEMIC CERTIFICATES/RESULT SLIP PAMOJA NA LEAVING CERTIFICATES) KIDATO CHA NNE, SITA NA VYUO.
2.VYETI HALISI VYA KUZALIWA (ORIGINAL BIRTH CERTIFICATES). HATI YA KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIKA.
3. MASHUKA MAWILI RANGI YA BLUU BAHARI (LIGHT BLUE)
4.CHANDARUA CHENYE UPANA FUTI TATU
5.NGUO ZA MICHEZO (TRACK SUIT NYEUSI,T-SHIRT BLUE NA RABA)
6.PASI YA MKAA.
7.NDOO MOJA.
8.PESA ZA KULIPIA BIMA YA AFYA KIASI CHA SHILINGI ELFU HAMSINI NA MIA NNE TU (50,400/=).
9.PESA KIDOGO YA KUJIKIMU.

ZINGATIA: KWA MUJIBU WA KANUNI ZA SHULE YA POLISI NI MARUFUKU KUFIKA SHULENI NA SIMU YA MKONONI. ATAKAYEPATIKANA NA SIMU ATAFUKUZWA SHULENI HAPO. SHULE ITAELEKEZA NA KUSAIDIA KUFANYA MAWASILIANO.
MAJINA YA WAHITIMU YANAPATIKANA KUPITIA TOVUTI www.policeforce.go.tz au WAFIKE OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Imesainiwa na:
 [AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.