Zaidi ya shahada 30 za kupigia kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu zimekamatwa na viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ) katika kata ya Somanda wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, huku watu ambao majina yao yanaonekana kwenye shahada hizo wakilalamika kitendo cha tume ya taifa ya uchaguzi ( NEC )kushindwa kudhibiti hali hiyo.
Katibu mwenezi wa chadema wilaya ya bariadi Martin Morga ameiambia ITV kwamba shahada hizo zimekamatwa katika kata za Somanda na Mhango zilizopo katika halmashauri ya mji wa bariadi na suala hilo tayari limefikishwa katika kituo cha polisi wilayani humo, huku kiongozi huyo akimtaka msimamizi wa uchaguzi jimbo la bariadi kuingilia kati suala hilo ili kuondoa uwezekano wa shahada hizo kutumika zaidi ya mara moja kupiga kura.
Baadhi ya wakazi wa mji wa bariadi ambao majina yao yamekutwa kwenye shahada zaidi ya moja,huku wenyewe wakikana kuzitambua wamedai kusikitishwa na hujuma hiyo kwani hali hiyo inaweza kuwatia matatani kwa vile ni kosa kisheria mtu mmoja kujiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari la kudumu la wapiga kura,huku kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa bariadi mathias mkumbo akisema ofisi yake haina taarifa za kukamatwa kwa shahada hizo bandia