MWENYEKITI wa chama cha DP Maendeleo Mch. Christopher Mtikila
amesema kuwa Umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) ni wasaliti na wamekuwa
vipande 30 vya fedha na kuwasaliti wananchi.
Alisema kuwa Ukawa walikula vipande 30 vya fedha na kuwa
hawajawahi kukanusha kuwa walikubaliana kuhusu katiba ya wananchi Pendekezwa ya
Watanzania kila Rais anavyo zungumza na waandishi wa habari mwisho wa mwezi
anasema kuwa anawashangaa ukawa na kuwa walikubaliana kuhusu katiba lakini
ukawa hawatoi tamko la kukanusa.
Aliyasema hayo akiwa Mkoani Njombe wakati Akizungumza na
wanachama wa chama hicho na kusema kuwa ukawa wamekula vipande vya fedha na
kuwasaliti wananchi na hasa kuhusiana ana katiba Pendekezwa ambayo ilisababisha
kuundwa kwa Umoja huo na kuwa yeye akiwa ni mmoja wa waanzilishi.
Alisema kuwa wananchi wamesalitiwa na Umoja huo kwa kuwa
umekaa kimya kila Rais anapo zungumza na wananchi mwisho wa mwezi na kusema
kuwa anawashangaa ukawa na kuwa walikubaliana.
“Rais anapo zingumza na waandishi wa habari kila mwisho wa
mwezi anasema kuwa anawashangaa ukawa kwa kuwa walisha malizana,” alisema na
kuongeza.
“Ukawa walikutana na Rais na kupewa pesa huko na kuondoka
usiku wa manane na kuwanyamazisha kisha kila mmoja kumsindikiza nyumbani kwake
na mzigo wa pesa aliopewa,” aliongeza Mch. Mtikila
Aidha Mch. Mtikila alisema kuwa kuna wanasheria wanao
shugulikia tatizo la kuondolewa katika kinyang’anyilo cha ugombea wa uraisi na
kusema kuwa kuna majaji wanao shughulikia suala lake kwa hati ya dharula na kuupeleka
tume ya uchaguzi.
Akisimulia mkasa na jinsi alivyo katwa alisema kuwa mgombea
mwenza alishindwa kufika kwa wakati baada ya mkewe kupata mshituko na kwenda
naye hospitalini.
Alisema mgombea mwenzake baada ya kupata nafuu aliwaambia
kuwa atakuja na Mtikila akaomba kuwa atachelewa kidogo mgombea mwenzake na
mahakamani aliapishwa na kuwa baada ya
mgombea wenzake huyo kutumiwa tiketi ya ndege alichelewa ndege na kwenda
kupanda meli ya Express na kufika kwa kuchelewa.
Alisema kuwa baada ya kuwasilisha suala lake kwa mahakamani
alisema kuwa mawakili waliwasilisha hilo na kuiambia tumekuwa alichelewa kwa
bahati mbaya lakini tume iliikata fomu yake.
Alisema jana mawakili wake wanaendelea vizuri na wamepeleka
hati ya dharura kwaajili ya kuirudisha jina lake kugombea nafasi ya urais.
Alisema kuwa anaimani jina lake lekirejeshwa atashina na
kusema kuwa wagombea urais wote ni mafisadi na kuwa mwaka huu CCM wamesimamisha
marais wawili kama alivyosema Mwenyekiti wa chama wananchi (CUF) Ibrahim
Lipumba.
Alisema kuwa mgombea wa urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema na kugombea kupitia Ukawa ameshindwa CCM na ndio maana amehamia huko baada ya kukosa nafasi katika chama
hicho.