MATOKEO katika jimbo la Makete Mkoani Njombe mbunge Binilith
Mahenge ameongeza katika kura za maoni zilizo fanyika juzi huku changamoto ya
miundombinu ikileta utata wa kutoa matokeo mapema.
Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpagike Akizungumza na Elimtaa alisema kuwa kutikana na changamoto za miundombinu ya jimbo la Makete
matokeo hayo jamemfikia usiku wa kuamukia jumatatu.
Alisema Katika jimbo hilo kulikuwa na wagombea watano
walliokuwa waking’ang’a kuchaguliwa na wananchi kuwakilicha chama chao katika
uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu mbunge wa jimbo hilo Binilith Mahenge alipata
kura 8534 Norman Sigala kura 8211, Bonic Muhami 500, Fabianus Mkingwa kura 466
na Lufunyo Rafael 226.
Alisema matokeo hayo kutoka jumamosi jioni yalikuwa
yakihesabiwa na kukusanywa kwa tabu kutokana na Jografia ya maeneo ya wilaya
hiyo.
“Kunamaeneo ambayo hayafikiki na kuwasilisha matokeo kwa
njia ya simu wanawasiwasi hivyo imewalazimu kupelkeka karatasi za matokeo
wazizo saini mawakala mpaka ofisi za wilaya,” alisema Mpagike.
Alisema kulingana na matokeo hayo Mahenge mbunge wa sasa
ndio ata ongoza katika majina yatakayo pelekwa katika kamati kuu ya CCM na
itarudisha jina tena kwaajili ya kuingizwa kwa wananchi kupigiwa kura.
Kwa matokeo hayo Wabunge wote walio kuwa madarakani wameshinda
kwa kishindo huku majimbo yaliyo gombewa na Wabunge waliokuwa wanatetea nafasi
zao ni manne ambayo Wabunge hao wameshindwa kwa kishindo.
Jimbo la Makambako lilikuwa chini ya Deo Sanga kura 7643 huku mgombea mwenzake akiwa
hajafika hata nusu ya kura zake, Alimwimike Sahi 499, na walikuwa wawili katika
jimbo hilo, jimbo la Ludewa kulikuwa na
Deo Filikunjombe ameshinda kwa kura 18290 huku akiwagaragaza wagombea wenzake
kwa kura nyingi ambao walikuwa watatu katika
jimbo hili na hata nusu hawajafikia.
Katika jimbo lingine ni la Njombe Magharibi lilikuwa na
chini ya Greison Lwenge ambaye alipata kura 13715 huku aliye mfuatia akijaribu
kumkaribia na alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla yake Thomas Nyimbo kura 2296
na mbunge mstaafu mwingine Yono Kevela 1900 na wengine wengine tisa wakitupiwa mbali
, Petro John, 467 Richard Magenga
417Abraham Chaula 382 Danford Mpumilwa 332, Hoseana Bumogero 322.
Majimbo mawili ya Njombe yanawagombea ubunge wapya ambayo ni
jimbo la Lupembe ambalo mshindi ni Joram Hongoli aliyepata kura 2233 huku
akiwatupa mbali wenzake walio kuwa nane Jeston Kaduma, 1912 Oska Msigwa, 1656 Emmanuel
Nyagawa, 1083 Avike Kyenga, 836 Lenda Hongoli, 471 Leila Malekela, 365 Osmondi
Malekela 103.
Aidha katika jimbo alilokuwa spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda
limepata mbunge mpya Edward Mwalongo kwa kupata kura 3870 ambapo saba walio
mfuatia walipambana na kuzidiwa kwa kura zaidi ya 1000 aliye mfufuata kupata
kura 2158 Lomanus Maemba Dioniol Msemwa 1676, Alnod Mtewele, 186, Alfred Luvanda
978, Laulian Mwaijinga 86, Hassan Mkwawa 152, Vitalis Konga 76.