Bvr njombe tena, uhakiki wa taarifa


HALMASHAURI ya wilaya ya Njombe imepokea mashine mbili za kuandikishia mpigakura kwa mfumo wa kierekroniki, (BVR) kwaajili ya kufanya marekebisho ya watu ambao walijiandikisha kupigakura na taarifa zao kukosewa.
  
Akizungumza ofisini kwake kaimu Mkurugenzi halmashauri ya mji wa Njombe na afisa utumishi Mbujilo Gwarbet, alisema kuwa halmashauri hiyo imepokea Bvr mbili kwaajili ya kufanya uhakika na kurekebisha wale ambao majina yao yatakuwa yamekokewa na kuwa ambao wamehama maeneo kurekebishiwa kulingana na na eneo alilopo.

Alisema kuwa kwa mashine hizo kila kata itapata mashine moja ambayo itakaa katika kata husika kwa muda wa siku tano ambapo mkazi wa eneo la kata hiyo ataenda katika ofisi ya kata ambapo mashine itakuwepo kwenda kufanya marekebisho.

“Mashine hizi zimekuja kwaajili ya kufanya marekebisho kwa watu ambao wanaona wamehama maeneo yao na kuona majina yalikosewa, au jina la kituo chake lilikosea watabadilisha lakini kwa wale ambao hawakujiandikisha hawata andikishwa labda kama kitambulisho kilipotea lakini alijiandikisha” alisema Gwalbet.

Alisema kuwa kwa wale ambao vitambulisho vilipotea watapewa vitambulisho vipya kwa kuvifuta katika orodha vile vya zamani na kuwa kama mtu alihama mkoa, kata ama mtaa atabadilishiwa taarifa na kuwekewa taarifa za kata aliyopo na kuwa itaangaliwa kama mwaka wa kuzaliwa ulikosewa..

Alisema mashine hizo kwa halmashauri yake zimeza kufanya kazi Ijumaa Augosti 7 ya mwishoni mwa wiki na itaendelea mpaka Septemba 10 na kuwa umeanza katika kata za Kifanya na Kihungilo ambapo mashine zitadumu kwa siku tano.

Baada ya kutoka katika kaza hizo na kumaliza siku tano mashene zitahamia katika kata za Makoho na Matola,zoezi litaanza Agosti 12 hadi 16, na kwa awamu ya tatuitakuwa ni kata za Lupondena Uwemba itakuwa ni Agosti 17 hadi 21 na Lugenge na Utalingolo Agosti 22 – 26,kata  Ihanga na Yakobi itakuwa Agosti 27- 31.

Aliongeza kuwa katika kata za Mjimwema na Ramadhani itakuwa ni Septemba 1 – 5 na kuwa zoezi hilo litamalizikia katika kata ya Njombe mjini Septemba 6 hadi 10 ambapo jimbo hilo la Njombe kusini litakuwa limemaliza uhakika wake kwa kata zote 13.

 Gwalbert alisema kuwa pia katika uhakika huo utakuwa unatoa watu ambao wamefariki katika Daftari na kuwato wale ambao wamepata matatizo ya kufungwa kuondolewa katika Daftari hilo.