IMEDAIWA kuwa huduma za ulinzi wa mtoto Mkoani Njombe zikafikia
ukomo baada ya wafadhili kujitoa, kutokana na fedha zilizopo kwa asilimia kubwa
kutoka kwa wafadhili.
Akizungumza katika kikao cha mw2aka cha tathimini ya ulinzi
wa mtoto mkoa wa Njombe, afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya
Njombe Justoni Chaula alisema kuwa kuna wasiwasi wa watoto kuto pata huduma ya
ulinzi kutokana na kuto kuwapo kwa fedha za kutosha kutoka ndani ya nchi
kwaajili ya ulinzi wa watoto.
Alisema kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali na
kupambana na wanao wanyanyasa watoto kutokana na vijiji vingi kuto kuwa na
polisi katika ofisi za kata na kutumia askali mgambo ambao wengi wao ni wazee.
Alisema kuwa licha ya kuwa na mgambo hao wazee kumekuwa na
kasumba ya watu wanao wanyanyasa watoto kutoroka katika mahali walipo hifadhiwa
baada ya kukamatwa.
Alisema kuwa licha ya kuwa na uhaba wa mahali pa kuwahifadhi
wahalifu dhidi ya watoto kumekuwa na changamoto za migamo hao waliopewa mafunzo
ya kuwadhibiti na kutambua uharifu dhidi ya watoto wamekuwa dhaifu kutokana na
umri wao na kushindwa kuwadhibiti waharifu.
Alisema ofisi yake inayo fadhiliwa na shirika la Umoja wa
mataifa linaloshughulikia watoto (Unicef) katika mradi wa ulizi wa watoto
wamekuwa wakiwasaidia kufika vijijini kutoa elimu juu ya ukatili na kuanzishwa timu
za ulinzi wa mtoto huku fedha kutoka serikalini kuto kuwepo katika shuguli
hizo.
Kutokana na kuto kuwapo kwa fedha za serikali anawasiwasi
baada ya kujitoa shirika hilo kuna uwezekano mkubwa wa kukwama kwa huduma hiyo.
Hivyo aliiomba serikali kuhakikisha kuwa kunakuwepo na vituo
vya polisi katika kata za mali na mijini ili kusaidia ulizi wa jamii na watoto.
Aidha Chaula alitaka tume ya ajira kuhakikisha kuwa inaajili
wafanyakazi wengi wa Maendeleo ya jamii ili kuisaidia jamii ya vijijini hasa
kulinda mtoto asipatwe na manyanyaso .
Akifungua mkutano huo kaimu katibu tawara mkoa wa Njombe Lameck
Noah alisema kuwa watoto wanahitaji upendo wa hali ya juu ili kuepusha jamii
yenye ukatili na visasi.
Alisema; “Mtoto anaye ishi kwa manyanyaso akikuwa anakuja
kuwa mtu hatari sana kwakuwa anaharibika kisaikolojia na kuwa na asili ya
ukatili mtupu lakini akilelewa katika malezi bora anakuwa na upendo wakati wate
atakapo kuwa mtu mzima,” alisema Noah.