Abiud Gamba mmoja wa menejimenti ya ACTN
Mkurugenzi wa ACTN Said Komwa
Washiriki wa mafunzo ya kuboresha kilimo mikoa mitatu ya
Njombe, Ruvuma na Iringa
WAKULIMA kutoka katika vikundi mbalimbali kutoka
halamashauri za Namtumbo, Songea vijijini Mkoani Ruvuma, Ludewa Mkoani Njombe na
halmashauri ya Kilolo Mkoani Iringa wametakiwa kuhakikisha wanahifadhi vizuri
mazao yao ili kuingiza katika ushindani wa soko la mazao yao na kuhakikisha
wanasafisha na kukausha vizuri.
Wito huo umetolewa na Meneja wa mradi uliofadhiliwa na AGRA, Frank Mhando inayojishughurisha na kuwasaidia wakulima kuinuka kiuchumi, kwa kuboresha mazao
yao kutoka kilimo hadi mavuno wakati wa semina kwa wakulima hao iliyotolewa na Taasisi
ya African Conservation Tillage Network, (ACTN) na kufanyika Njombe mjini.
Alisema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakilalamika masoko
hamna kitu kinacho shusha bei ya mazao ni kutokana na kuto kuwapo kwa utunzaji
bora wa mazao na kushindwa kuyaweka katika hali ya usafi.
Mhando alisema kuwa wakulima wengi wamekluwa wakaweka mazao
yao katika hali ya uchafu kitu kinacho wakimbiza wanunuzo na kuleta malalamini
ya kuto nunuliwa kwa mazao hayo.
Alisema kuwa; “Wakulima wamekuwa walikusanya mahidi yaliyo
vunjika vunjika na mazuri kitu kinacho kimbiza wateja kwani nao wakinunua kwako
watashindwa kuuza kwa kuwa sio masafi, lakini kama utaweka katika hali ya usafi
utaweza kupoata wateja kwa bei nzuri.
Aidha kwa upande wao wakulima kutoka Songea Vijijivi, Namtumbo, Ludewa
na Kilolo wamesema kuwa kwa kupata elimu hiyo waliyo itata wataendeleza kilimo
chao kwa kwenda kufuiata kanuni za uhifadhi, usafi wa mazao, na kulima kilimo
hifadhi ili mashamba yao kuwa imara na kurutubika.
Wamesema kupitia elimu hiyo wataenda kuielimisha na jamii
inayo wazunguka ili nako kujitahidi kulima kilimo hifadhi na kuweka safi mazao
yao kwa kuhufadhi bira kuweka viwatilifu vya maji ili kuwa na mazao yenye
usalama.
Akifunga mkutano huo Mkurugenzi wa ACTN, Said Komwa alisema
kuwa wakulima wajitahitu kulima kilimo hifadhi kwaajili ya kujipatia kipato
maradufu ya wanavyo pata sasa na kuwa kilimo hifadhi hulinda shamba na kusisitiza
kuchambua mazao yao ili mnunuzi asipate mashaka na mazao yao.
Alisema kuwa wakulina wanawajibu wa kuhufadhi kwa pamoja
mazao yao ili kupata wateja wa jumla kuliko kuuza mazao mmoja mmoja na hatimaye
kufikia malengo yao ya kuwa na maisha bora.