HARMASHAURI MKOANI NJOMBE ZATAKIWA KUJENGA USHIRIKIANO

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Akizungumza Katika Mkutano Mkuu wa NJOCOBA wa Wanahisa

MKUU wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi ametoa agizo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote mkoa huo kuhakikisha zina ushirikiano mzuri kwa benki ya wananchi Njombe kwa kuwa ndio inayo saidia wananchi wenye halmashauri hizo kwa mikopo ya kilimo.

Akizungumza katika mkutano wa wanahisa wa benki ya wananchi Njombe (Njocoba) mkoa wa Njombe alisema kuwa benki hiyo ni ya wananchi mkoa huo hivyo halmashauri zinatakiwa kuwa na ushirikiano na benki hiyo ili kuimalisha benki inayo wasaidia wananchi wa halmashauri zao.

“Ras fuatilia wakurugenzi wa halmashauri ambao hawana ushirikiano wa kweli na benki hii ya wananchi wao kwa sababu ndio inayo wapatia wakulima mikopo na kuinua halmashauri zetu,” alisema Dkt. Nchimbi.
Alisema kuwa haitapendeza halmashauri haina ushirikiano wa kweli na benki inayo wasaidia wakulima na wakazi wa halmashauri zao.

Alitaka benki hiyo kuwalea wakulima wao ambao wanakopa kutitia benki hiyo na hasa kwa kuwapatia elimu ya mikopo ili kukabiliana na tatizo la kuto lejesha mikopo kwa wakati.

Alisema kuwa benki inatakiwa kuwa ya tofauti na benki zingine zote na hasa kwa kuwa na dawadi la wakulima ili kutoa elimu kwa wakulima wanaokopa mikopo na kujua matumizi sahihi ya mikopo yao.

Alisema kuwa haitapendeza kuona mkopaji wa mkopo anakopa pesa na kuzipeleka katika mambo ambayo hayakuwepo katika malenho yake ili kulina na uulejesha kwa wakati.

Nchimbi alisema kuwa dawati hilo litasaidia wananchi kulina mkopo kwa kuto peleka mikopo yao katika harusi, Kicheni pani na michango ya sherehe kwa kuwa michango hiyo haileti Maendeleo.

“Kuna watu wanakopa mikopo katika kicheni pati kwa kulenga kuwafuraisha watu walio waalika na kujikuta wakishindwa kulejesha kwa kuwa harusi haziwezi kuzarisha,” aliongeza Nchimbi.

Aliongeza kuwa benki ili kuwa na ukuaji na kuongeza wateja ni lazima ikawa inatoa ajira kwa wazawa wa mkoa wa Njombe ili kusaidia kuongeza wanachama kwa kuona watoto wao wanafanya kazi benki hiyo na kujiunga kuliko kuajiri watu kutoka nje ya mkoa wa Njombe na wakazi wa mkoa wa Njombe wataona benki hiyo ni yao.

Aidha akisoma taarifa ya benki hiyo Menyekiti wa bodi Yohana Kalinga,  alisema kuwa benki hiyo inapambana na wadaiwa sugu ambao hawajalejesha mikopo ili kuhakikisha benki hiyo inasonga mbele na kuwa mikopo isiyo rejeshwa huathiri ukuaji wa benki.


Alisema kuwa anaomba halmashauri za mkoa wa Njombe kuwa na ushirikiano na benki hiyo ili kuhakikisha kuwa benki hiyo inaimalisha wananchi wanao jiunga kila siku ka mikopo ya kilimo.