WANANCHI wa kijiji cha Idundilanga ambacho kwa sasa ni mtaa
wameamua kuirudisha hospitali iuliyojengwa kwa nguvu zao enzi za utawala wa
chama kimoja kwa kuwa inadaiwa kutaka kumilikiwa na chama tawala cha CCM.
Hospitali hiyo iliyojengwa na wananchi Miaka ya chama kimoja
na majengo ya biashara ambayo yapo kuziunguka hospitali hiyo ambapo baada ya
mtaa huo kwa sasa upo chini ya mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo,
(Chadema) imedaiwa mapato hukusanywa na chama tawala.
Wananchi hao wa kijiji cha Idundilanga ambacho kwa sasa ni
mtaa na kukusanya wananchi kutoka mitaa ya Mpechi, Joshoni ambayo awali ilikuwa
katika kijiji hicho na kuhusika katika ujenzi wa hospitali hiyo Juzi walifikia
maamuzi ya kuirudisha hospitali hiyo kwa wananchi wa mtaa huo.
Katika mkutano huo ambao ulihudhuliwa na Diwani wa kata ya
Njombe Mjini ambapo mtaa huo wenye hospitali, Agley Mtambo na uongozi wa
serikali ya mtaa akiwemo mtendaji wa mtaa huo pamoja na wananchi baada ya mtaa
wao kukabidhiwa kwa mwenyekiti mpya walishangwaza na kodi za biashara zilizopo
katika majengo ya eneo hilo kuchukuliwa na Chama tawala badala ya serikali ya
mtaa.
Mwenyekiti wa mtaa huo katika mkutano wa dharula wa hadhara
Lameck Ulaya alisema kuwa ameamua kuuitisha mkutano huo kwa lengo la
kuwajulisha wananchi kinachoendelea katika majengo waliyojenga wenyewe sasa
kumilikiwa na chama cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kuwa wakati anakabidhiwa ofisi yake alishangazwa na
mapato ya wapangaji majengo kuzunguka katika hospitali ya Idundilanga
kuchukuliwa na CCM wakati eneo hilo lilijengwa na wananchi na mapato ya eneo
hilo ilitakiwa kufanya Maendeleo ya wananchi.
“Katika mkutano huu wa dharula ilitakiwa kuwapo kwa viongozi
wa CCM kutoka maeneo ambayo zamani ilikuwa ni kijiji cha Idundilanga na
wananchi wake lakini hawajafika katika mkutano huu hivyo nawaachia wananchi
kutoa maauzi juu ya hospitali na eneo hili,” alisema Ulaya
Wananchi wa mtaa huo kwa pamoja waliamua eneo hilo kuwa
chini ya wananchi na kuanza ujenzi wa hospitali ya mtaa ambayo itakuwa ya kisasa
na kuwahudumia wananchi kwa gharama nafuu ambapo majengo yanayozunguka
hospitali hiyo yatavunjwa kisha ujenzi kuanza.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Mtambo alisema kuwa
alitarajia katika mkutano huo kuwapo afisa ardhi wa halmashauri kwa bahati
mbaya hakuwepo na kuwa baada ya kufikiwa maamuzi hayo mtaa na kata watafuatilia
hati ya ardhi ya eneo hiyo ili kuepusha utata miaka ya hapo baadae.
Mtambo alisema kuwa katika eneo hilo kutabomolewa na kisha
kuaza kwa ujenzi wa hospitali ya kisasa na kuwa wananchi katika hospitali hiyo
watachangia huduma kidogo kama hospitali ya serikali na sio kama hospitali ya mtu
binafsi.
“Majengo yanayozunguka Hospitali hii yatavunjwa na kisha
kuanza ujenzi wa hospitali na kwa kuwa hii itakuwa ni hospitali ya wananchi
dawa zitaletwa na serikali na wananchi mtalipia kiwango kidogo cha huduma,”
aliongeza Mtambo