Wakulima waogopa mokopo

BAADHI ya wananchi wamedaiwa kuogopa mikopo kutoka halmashauri  ya Mji Njombe wasesema kuwa pesa hizo ni dili na kuogopa kutumia fulsha hiyo.

Akizungumza wakati wa matembezi ya mafunzo baada ya mafunzo ya ndani ya kilimo biashara na utunzaji wa mazingila ambacho kimetolewa na taasisi ya Forum CC kwa kushirikiana na taasisi ya Seco Njombe, afisa mtendaji wa kata ya Luponde, Stanley Mkondola alisema kuwa wananchi kwa sasa wamekuwa waoga kuchukua mikopo kutoka halmashauri.

Alisema kuwa wananchi wasiogope kuchukua mikopo na kuwasihi kutumia fursa ya mikopo na kukumbuka kuresha mikopo hiyo.

Alisema kuwa wananchi walio na uelewa wanaotakiwa kuonyesha mfano katika uoneshaji wa vitendo katika kilimo biashara ambapo watawashawishi na walio katamaa.

Nao wakulima kutoka katika kata Mbalimbali wakiwakilishwa na Panusi Mgaya amesema kuwa walisha wahi kuchukua mkopo na kuwa walipo ingia katika mikikopo walikatishwa tama kama anavyo eleza.

Alisema wanancho wamekuwa wakiogopa kutokana na kuna mwaka waliingia watu na kushawishi kujiunga na hawakuona matokeo yake na kuogopa kabisa wakisikia Sacoss.

"Wakulima wanaogopa na wanapo sikia ukishindwa kulipa mkopo unafungwa hivyo wanaogopa sana kuingia katika mikopo," alisema Mgaya

Naye afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya mji Yohana Kalinga amesema kuwa serikali imeandaa mkopo kwa wakazi wa kata mbalimbali zitakazo onyesha mwitikio wa kufanya Maendeleo.

Alisema kuwa mwenge wa mwaka huu utakapo pita katika halmashauri ya Mji njombe kunatarajiwa kutolewa milioni 20 kwa wakulima.

Seco ikiwakilishwa na mkurugezi wake Luka Mgaya alisema kuwa taasisi hiyo ita ungana na Forum CC kwa kuwawezesha wananchi watakao onyesha uwezo baada ya kupata mafunzo hayo.