WAKAZI kutoka sehemu Mbalimbali za mkoa wa Njombe wamewalalamikia wafanyabiashara
waliofunga maduka yao kwa siku nzima ya jana kwa kuwa hawakuwapa taarifa ya
kufungwa kwa maduka wakati wametumia gharama kufuatia bidhaa.
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka wilaya ya Mkoa wa Njombe ambao
walikuja mjini hapa kwaajili ya kujumua bidhaa wamelalamikia kitendo cha
kufungwa kwa maduka bila ya wao kuwa na taarifa.
Nikolas Mahundi mkazi wa wilayani Ludewa alisema kuwa ametoka
wilayani kwake akitegemea kukuta maduka yakiwa wazi na kununua bidhaa kwa ajili
ya duka lake lakini alicho kutatana nacho ni makufuri katika maduka ambayo
amekuwa akinunua bidhaa za jumla.
Alisema kuwa wafanyabiashara ni bora wakawa wanatoa taarifa
ili wasitumie gharama kuja mjini na kuwa sasa wamewaongizea gharama kwa kuwa wanahitajika
kulala kwa kuwa hakuna gari inayoenda wilayani huko ikifika majira ya jioni.
Alisema kuwa angekuwa na taarifa asinge kuja mjini na kuwa
hiyo ni adhabu kwao licha ya kuwa wamefunga kwa malengo mazuri.
“Kufungwa kwa maduka tuwe tunapata taarifa na sisi wenzenu
ili tusije tunapo kuja huku na kukuta madrka yamefungwa mtatutesa wenzenu
jamani,” alisema Mahundi
Naye Jonasan Sanga mkazi wa wilayani Makete alisema kuwa kufungwa
kwa maduka kumemuongezea gharama ya kulala mjini Njombe wakati alitakiwa kufika
na kujumua mziko kisha kurudi.
Alisema kuwa wafanyabiashara ni bora kama wanataka kufunga
maduka siku moja kabla wakiwa wanatangaza ili wanao toka wilayani wasije mjini.
Wafanyabiashara Mkoani Njombe wamefunga maduka kwa lengo la
kusikiliza kesi ya Mfanyabiashara mwenzao Jonson Minja ambaye kesi yake
inasikilizwa tena jana Mkoani Dodoma na kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakifunga
maduka kila siku ya kusikiliza kesi hiyo.
Kwa upande wa viongozi wa wafanyabiashara walisema
watalizungunzia suala la kufunga kwa maduka baada ya kufanya mawasiliano na
kuwa watawajulisha wanahabari.
Picha na Elimtaa Photographer