MTEMVU ATATUA MGOGORO YA MIKATABA KWA WANANCHI WA MTA WA CHAUREMBO, KURASINI JIJINI DAR

 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na wananchi wa kijiji Chawavuvi Mta wa Chaurembo uliyopo Kurasini baada ya kutokea mwekezaji na kuwa na sinto fahamu ya muda mrefu na kupelekea wananchi kufanya maandamano ya amani hadi Ofisi za Serikali ya Mta huo na kumlazimu Mbunge kuingilia kati mgogoro huo  Dar es Salaam leo (PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA)
  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu  akipitia moja ya mkataba waliyoandikiwa wananchi hao na mwekezaji ambayo wananchi hao hawajaridhishwa, Muhandisi Msaidizi wa Bandari  na kiongozi wa kero za wananchi wa kijiji Chawavuvi Mta wa Chaurembo Kurasini David Mlassi akimweleza mambo fulani mbunge huyo (kushoto)
 Wananchi wa kijiji cha Wavuvi wa Mta wa  Chaurembo wakimsikiliza Mbunge huyo.
 Wananchi wa kijiji wa Chaurembo wakipiga makofi baada ya  Mbunge huyo kuongea jambo
 Wananchi wakimsikiliza  kwa makini Mbunge wao alipokuwa akizungumza jambo
 Wananchi wakiimba na kufurahi baada ya Mbunge wa jimbo la Temeke kutatua na kusikiliza kero zao
Nifuraha kwenda mbele wakidai walikuwa hawana amani na vitisho walivyokuwa wakivipata na kutakiwa kusaini mikataba kwa vitisho