Tuzo ya Taaluma yatolewa kmwa mara ya kwanza

BAADHI ya wanafunzi mkoani Njombe hawajui kuimba wimbo wa taifa na hivyo kuboronga walipo imba wimbo huo mbele ya mkuu wa mkoa wakati wa uzindizi wa tuzo ya elimu ya mkuu wa mkoa.

Wakiimba wimbo huo kwa kupishana beti katika uzinduzi wa tuzo hiyo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wangine wakisema Mungu ibariki Afrika wenzao wanasema Mumgu Ibariki Tanzania.

Mkanganyiko huo ulitokea wakati wa ufunguzi wa hafla ya uzinduzi wa tuzo ya taaluma ya mkuu wa Mkoa ambayo ni kwa  mara ya kwanza kutolea mkoani na nyanda za juu kusini.

Wanafunzi hao waliimba hivi  “Mungu ibariki Afrikaa na wengine Mungu ibariki Tanzaniaa kwa pamoja,” walisikika.

Uzinduzi wa tuzo hiyo uliendana kutolewa kwa taarifa ya elimu ya mkoa wa Njombe ambapo zaidi ya wanafunzi 3500 wanashindwa kufika darasa la saba kwa mwaka kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo ya utoro na vifo.

Akisoma taarifa ya elimu ya mkoa wa Njombe Ofisa elim u mkoa wa Njombe Said Nyasiro alisema kuwa wanafunzi zaidi ya asilimia 20 ya wanafunzi wanaonza darasa la kwanza hushindwa kufifika darasa la saba.

Alisema kuwa wanafunzi wasio hitimu kidato cha nne ni zaidi ya wale wanao shindwa kufika darasa la saba ambapo kwa sekondari ni asilimia 40.

Akizungumzia tuzo hiyo mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi alisema kuwa tuzo hiyo inalengo la kuongeza ufauru kwa wanafunzi wa mkoa huo na kuuweka hamasa kwa walimu kuongeza juhudi.

Dkt Nchimbi alisema kuwa tuzo hiyo inalenga kufanya mkoa wa Njombe kushika nafasi ya kwanza kitaifa wakati kwa mwaka wa jana mkoa huo ulishika nafasi ya tano kitaifa.

Hamasa kwa wanafunzi na walimu ilikuwa ni zawadi mbalimbali huku shule zilizofanyavizuri nne zikipata zawadi ya Pikipiki, kwaajili ya kurahisisha utendaji wa wakazi kwa shule hizo na kuzishawishi na shule zingine kujitahidi kufanya vizuri.

Kwa upande wa mmoja wa walimu ambao shule zao zimepata zawadi ya Pikipiki na kutakiwa kusajili kwa jina la shule, Mwalimu Lenatus Njooka alisema kuwa wamekuwa wakikwama pale wanapotakiwa kufika mjini kwa ajili ya mahitaji ya shule.

Alisema kuwa shule yake awali ilikuwa na walimu watatu na kuwa baada ya kuongezwa kwa walimu katika shule hiyo walijitahidi kufundisha wanafunzi  na hatimaye shule yake ya Iduchu kushika nafasi ya juu na kupata zawadi hiyo.

Aidha baadhi ya wakazi wa Mkoani Njombe wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya kuanzishwa kwa tuzo hiyo na kuwa hakuna uhusiano mzuri baina ya wazazi na walimu.

Hivyo walitoa ushauri kwa mkoa wa Njombe kuhakikisha kuwa unapo taka kufanikiwa katika elimu ni lazima kukawepo muunganiko mzuri baina ya wazazi na walimu ili kuongeza ufauru.


 Afisa elimu mkoa wa Njombe, Said Nyasilo wa Pili kushoto.

 maandamano ya wanafunzi
Mkuu wa Mkoa wa Njombe DR. Rehema Nchimbi wakwanza kushoto akitazama maonyesho ya kitaaluma