NJOCOBA KUMLIPA MTEJA WAO MILIONI 20

  • Mkataba wa mkopo ulivunjwa


MAHAKAMA ya hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoani Njombe imeiamuru benki ya wananchi Njocoba kumlipa shilingi milioni 20, aliyekuwa mteja wao kwa kmuvunja mkataba wa mkopo kama fidia ya usumbufu na kuuza mali zake alizo weka kama dhamana ya mkopo wake.

Mteja huyo   Jane Mganwa aliipandesha benki hiyo mahakamani kwa kuvunja mkataba akiwa na lengo la kulipwa fidia na benki hiyo kwa kumfanyia vurugu na kuvunja mkataba walioandikiana wakati anachukua mkopo.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo yenye namba 7/2013 hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi wa makahakama hiyo, John Kapokolo alisema kuwa mdai ambaye alikuwa ni mteja wa benki ya Njocoba katika mkopo alifungua kesi hiyo mwaka 2013 akidai fidia ya kunyanyaswa  dhidi ya benki kiasi cha shilingi milioni 50.

Alisema kuwa mahakama hiyo imesikiliza kesi ya ushahidi upande wa mdai na mdaiwa na kuona Jani ana haki ya kulipwa pesa hizo kama fidia ya kufanyuwa unyanyasaji na kuuzwa vitu vyake kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa mkopo.

Alisema kuwa baada ya Mahakama kujiridhisha imeona mdai atalipwa pesa hizo na kuwa kuanzia siku ya hukumu mdai atatakiwa kulipwa fidia hiyo na kuwa rufaa ya kesi hiyo ipo wazi ndani ya siku 30.

Akisoma maelezo ya kesi hiyo Hakimu Kapokolo alisema kuwa mdai Jane alikopa kutoka katika benki hiyo mwaka 2012 mwezi juni na mkataba ulikuwa unasema anatakiwa kulipa kila wiki pesa na kuwa alilipa kwa muda wa miezi miwili na baada ya hapo alikutanan na Meneja kumuomba kuwa atashindwa kurejesha pesa hizo kwa kuwa alikuwa anauguza baba yake.

Alisema kuwa mdai baada ya kuomba kuto peleka pesa hizo benki ililipo ona pesa za mteja wao hazipelekwi ilitafuta dalali na kwenda kuuza mali zake ambapo inadaiwa kuwa ziliuza luninga, vyombo vya nyumbani, vitanda na vitu mbalimbali ambavyo aliweka kama dhamana ya mkopo ikiwa ni pamoja na sehemu yake ya biashara.

Ukisomwa mkataba wa kuchukua pesa hizo uliowekwa na benki hiyo na hakimu ambao uliwekwa mahakamani hapo kama kielelezo ulikuwa unasema kuwa mdaiwa atatakiwa kuchukuliwa pesa zake ambazo anaweka katika vkikundi chake na kama hazitatosha itatakiwa kuuzwa vitu vyake.

“Mkataba ambao uliwekwa mahakamani hapa kama moja ya ushahidi katika kesi mkataba huo unasema kuwa mkopaji kama atashindwa kulipa atatakiwa kuulizwa na kisha kama atashindwa vitu vyake vitauzwa,” alisema Hakimu Kapokolo.

Mahakama ilitoa ushauri kwa vyama vya mikopo kuto fanya maamuzi ya haraka kwa wakopaji wao na kujua matatizo ya wateja wao kabla ya kuuza vitu vyao.

Aidha mahakama iliona mshitakiwa ambaye ni benki itatakiwa kulipa pesa mdai huyo shilingi milioni 20 kwa lengo la kumfidia kwa fedheha alizozipata, mali zilizouzwa na kuwa baada ya kuuzwa kwa vitu vyake.