MKUTANO WA TAKWIMU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM


Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),kutokaTanzania Dkt. Albina Chuwa akifungua mkutano wa Wakurugenzi na Watalaam wa Takwimu kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili mausuala mbalimbali ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Uganda Bw. Ben Mungyereza akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwi mu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashari kikuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Rwanda Bw. Yusuf Murangwa akitoa mchango wake kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa matumizi ya Takwimu baina ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisiya Takwimu Kenya Bw.Zachary Mwangi akizungumza na washiriki wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Burundi Bi. Jeanine Niyukuri akichangia wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afriki Mashariki uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi yaWashiriki wa Mkutano waWataalam wa Takwimu wanchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashari ki wakifuatilia mausuala mbalimbali wakati wa Mkutano huo leo jijini Dar es salaam. 

Na. Veronica Kazimoto,

Wakurugenzi Wakuu wa Ofisi za Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na Tanzania wamekutana leo  jijini Dar es salaam kujadili mchango wa matumizi ya Takwimu sahihi katika kuleta maendeleo na kukuza ushirikiano baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

Akifungua Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa mkutano huo pamoja na mambo mengine unazileta pamoja Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali ya Takwimu na mchango wake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi hizo.

Amesema kuwa mkutano huo umelenga kuongeza na kuimarisha ushirikiano baina ya Nchi Wananchama wa Jumuiya hiyo katika matumizi ya Takwimu pamoja na kupitia mabadiliko ya sheria mbalimbali zinazosimamia masuala ya Takwimu kwa Nchi Wanachama.

Kwa upande wao wakurugenzi hao kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, na Burundi wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania kunatoa matumaini ya mwendelezo wa ushirikiano katika matumizi ya takwimu sahihi kutokana na mchango wake katika maendeleo ya nchi zao na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.

Wamesema kuwa nchi zao zitaendelea kushirikiana kikamilifu katika kuhakikisha kuwa kunakuwa na usimamizi mzuri wa takwimu mbalimbali zikiwemo za kilimo, Viwanda, Biashara, uchumi  na takwimu nyingine kwa manufaa ya wananchi wa Jumuiya hiyo.


Kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania ambao umehusisha wakurugenzi wakuu, wakurugenzi na maafisa wandamizi wa takwimu ni mwendelezo wa mikutano mbalimbali inayofanyika katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kujadili mchango wa matumizi ya Takwimu sahihi katika kuleta maendeleo na kukuza ushirikiano baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

by Michuzi-Matukio