Man Utd yazimwa Goodison Park




LIVERPOOL: JAIZMELEO
Kocha Louis Van Gaal akishindwa kuamini kilichotokea Goodison Park. (Picha na Daily Mail)
Ashley Young akipambana vikali na Lennon aliyetolewa kwa mkopo na Tottenham
  
Msimu uliopita katika mechi kama hiyo
David Moyes alijikuta katika wakati mgumu,
mwangalie shabiki anachokifanya
HII ndio Ligi Kuu ya England (EPL), huwezi kuamini kama Manchester United imebanjuliwa mabao 3-0 na Everton.

Ushindi huo wa Everton umemweka kocha Louis Van Gaal katika wakati mgumu huku wachambuzi mbalimbali waliokuwa wakiisifia Man Utd kubaki midomo wazi.

Everton walifungua ukurasa kupitia kwa James McCarthy dakika ya 5, John Stones dakika ya 35 na dakika ya 74 Kevin Mirallas akitokea benchi aliifungia Toffees bao muhimu.

Kwa matokeo hayo Everton imekaa katika nafasi ya 10 ikiwa na alama 44 ikitanguliwa na Stoke, Swansea, Southampton, Spurs na Liverpool.

Matokeo mengine ni Liverpool ilikubali kutoka sare tasa dhidi ya West Brom huku Manchester City wakiidungua Aston Villa mabao 3-2.