DIWANI WA KATA YA UYOGO PAUL MAGAZI NA WENZAKE 5 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA ZA HALMASHAURI.

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA KAHAMA PAUL MAGAZI.

Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini Tanzania (TAKUKURU) wilayani Kahama  mkoani Shinyanga imewafikisha katika mahakama ya wilaya watuhumiwa 6 kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya Udanganyifu.

Watuhumiwa hao ni Paulo Magazi diwani wa kata ya Uyugo (CCM), Zuberi Dokezi,Juma Itengeshi, Edward Kalikali, Chirstina Ntelya na Yosidi Nyanda ambao wote  kwa pamoja wakiwa ni wakazi  mjini kahama.

Imedaiwa Mahakamani hapo kuwa mnamo October 13 mwaka 2009 watumiwa hao walijipatia fedha kiasi cha sh,  laki 1 na elfu 60 kwanjia isiyo halali kwa kughushi nyaraka za serikali katika kikao cha Baraza la madiwani wilayani humo.

Akisoma maelezo ya kesi hiyo mwendeshamashitaka wa Takukuru  Osboni Paissi mbele ya hakimu wa mahakama hiyo George Mariki amesema kuwa watuhumiwa hao 6 walijipatia fedha za posho za vikao vya baraza la madiwa isivyo halali.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kughushi nyaraka za serikali kwa kushirikiana na Christina Ntelya ambaye hapo awali alikuwa ni mhasibu wa halmashauri ya wilaya ya kahama anayedaiwa kutoa fedha hizo.


Hata hivyo Watuhumiwa hao 6 wamekana shitaka linalowakabili na kufanya kesi hiyo kuahirishwa mpaka may 8 mwaka huu ampapo itatajwa tena mahakamani hapo.