ZOEZI la uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura kwa
mfumo wa kielektroniki (BVR) limeingia katika hatua ya mwisho mkoani Njombe
tangu lilipo zinduliwa Februari 24 katika halmashauri ya mji wa makambako
na kisha kusambaa katika halmashauri zote za mkoa huo.
Uandikishwaji huo uliingia katika wiki ya mwisho Aprili 9 na
litadumu katika kata hizo ambazo ni za mwisho na unatarajia kumalizika Aprili
15 mwaka huu.
Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe kata mbili ambazo zimeanza
mwishoni wiki iliyopita na kumalizika Aprili 15 kwa mji wa Njombe, na zimeanza
kata mbili za mwisho za Njombe Mjini na Ramadhani.
Elimtaa ilizuru katika vituo mbalimbali ndani ya kata za Njombe
Mjini na Ramadhani hususani vituo vilivyopo mitaa ya Kibena na
Idundilanga na kujionea foleni ndefu ambayo bado imeendelea kuzua
malalamiko.
Baadhi ya wakazi ambao wanaiomba tume kubadili ratiba ya
kufungua vituo kwani wamekuwa wakifika usiku kujiandikisha huku vituo
vikifunguliwa saa mbili kama ilivyopangwa kwa kuwa wananchi wamekuwa wakiwahi
asubuhi na kukaa kwa muda mrefu mpaka kufika saa mbili.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Idundilianga, Lameck Ulaya ambao
una jumla ya vituo vinne ya kuandikisha na ambaye alisema huenda
wananchi wakawa na dhamira ya dhati katika kuwapata viongozi wao.
Alisema kuwa wananchi wake wamehamasika kushiriki katika
uandikishwaji katika daftari hilo ili kushiriki na kuwapata viongozi wao
ifikapo Oktoba kutokana na mwamko mkubwa wa jamii kujitokeza katika vituo
vyao pamoja na kuhimiza wananchi wengi kuendelea kujitokeza.
Zoezi hilo katika kata za Njombe mjini linaonekana kuwa na
mafanikio makubwa kutokana na tume kuamua kuwatumia waandikishaji kutoka kata
nyingine na hivyo wanauzoefu na mashine za BVR ambapo zaidi ya watu 150 katika
vituo kwa kila kituo kwa siku moja huandikishwa.