Chadema Waunguruma kwa Japipo, kwawaka moto


 Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar akiwasili katika viwanja vya shule ya Azimio mjini Makambako Leo

 Wakazi wa mko wa Makambako wakisikiliza viongozi wa Chama Chadema katika mkutano wa Salum Mwalimu akiwa katika Ziara yake mkoani Njombe

Nassari alitua Makambako, Njombe
Kasambala  Joseph Alipata nafasi ya kusema yake ni mjumbe wa baraza kuu la Chadema

wakazi wa Makambako wakikubari jambo

Makambako pipooooz......... powaaaaaaaa!!!!
Nassari, Mwalim wakiteja jambo kabla ya kupanda jukwaana Makambako

Lulandala akisisitiza jambo ambaya ni katibu wa Chadema mkoa wa Njombe
Ilifika zamu ya Nassari kutema cheche za maana kwa wakazi wa Makambako

Salum Mwalimu nae akalivaa jukwaa na kusema yake



Makambako pipoooooz


POLISI mji mdogo wa Makambako imetupiwa lawama ya kuhamisha mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuhofia kujibiwa Zitto Kabwe na Chama hicho katika mkutano wake mjini humo.



Akizungumza katika mkutano wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar Salum Mwalim alisema kuwa polisi wameongipa chadema kumjibu Zitto na kuuhamisha mkutano ili wakose watu.

Alisema kuwa licha ya kuhamishwa kwa mkutano wao wamepata watu rukuki na kuwa hawakuwa na mpango wa kumzungumzia Zitto kwa kuwa zito ni mtu mdogo sana katika chama hicho.

Mwalimu ambaye amehitimisha ziara yake nyanda za juu kusini ambapo alianzia mkoani Rukwa, akipita Mbeya, Njombe Ruvuma na kumalizia Makambako alisema kuwa ziara hiyo ililenga kufungua mikutano ya mafunzo ya viongozi.

Amewataka jeshi la Polisi kuhakikisha wanatenda haki kwa vyama vyote hapa nchini na si CCM, Chadema wala TLP ili kulejesha imani yao ya wakati ule wa IGP Said Mwema Ambaye alianzisha Polisi jamii.

Alisema Polisi jamii imeanza kupotea kwa watu kutokana na Jeshihilo kufuata kauli kutoka kwa viongozi wa CCM na kukandamiza watu wengine na vyama vingine vya siasa.

Alisema kuwa kuhusu watu kujiandikisha Chama cha Mapinduzi kilitaka kucheza Penati kwa kuwaandikisha watu wachache kwa kuingia katika uandikishwaji bila kuwataarifu wananchi lakini chama chake kiliusoma mchezi na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.

Alisema kwa tume ilianza mkoani humo ikiwa na lengo la kumaliza mkoa wa Njombe na kuingia katika mikoa mingine ikiwa na matumaini ya kupiga kura ya maoni Katiba pendekezwa.

Alisema kuwa walihamasisha wananchi mpaka tume wakashindwa kumaliza uandikishwaji kwa wakati kutokana na wingi wa wananchi waliokuwa wajijitokeza kuandikishwa.

Mwalimu alisema kuwa walitumia njia ya kupita nyumba kwa nyumba kuhamasisha na kusababisha mamia kwa maelfu kumiminika katika vituo vya kujiandikisha.

Alisema kuwa mikoa mingine inawapongeza wakazi wa mkoa wa Njombe kwa kujitokeza kwa wingi na kuwa wamepata funzo kutoka mkoa huo na kuwa itakapo fika zau yao watajitokeza kwa wingi.

"CCM wamekuwa wakifanya ujanja katika uandikishwaji sasa janja yao tuliigundua wakati daftari linaanza kuandikishwa mkioani njombe tume ilijia itapiga fastafasta mkoani njombe na kumaliza mikoa mingine fasta kwakuwaandikisha watu wachache wakini wameshindwa," alisema Mwalim 

Naye mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari alisema kuwa Njombe ya sasa sio nyombe ya mwaka 2010 ambayo ilimchangua mbunge wa CCM ambaye alicheza mziki bungeni.

Alisema kuwa anashangaa kuona watanzania wakiteseka wakati kuna watu wanaiba mabilioni ya pesa na atashangaa sana kuona watanzania walio shuhudia pesha nyingi zikiibwa katika masakata ya Escrow, Epa na mengine kama ya Rada wakichagua tena chama hicho.

alisema kuwa Chadema kimekuja kuwakomboa watanzania katika masakata ya kuipiwa pesa zao na kuwa hatopenda kuona miaka ijayo ya 2016 wananchi wakiteseka kupata huduma kama maji, na huduma za afya na wabunge wakila bata Dodoma na Dar es salaam.

alisema kuwa Chadema ikichukua nchi atamuomba laishi kumpa yeye cheo kwa mda wa mwezi mmoja tu wa Novemba na kuwa naibu waziri wa mambo ya ndani ili nao polisi wanufaike na kuwahoji walivyo watesa walivyo kuwa wapinzani.


Aidha mjumbe wa baraza kuu la Taifa la Chadema Kasambala Joseph alisema kuwa kutokana na tukio la kuhamisha kutoka Uwanja wa Polisi Ambao wamekuwa wakifanyia mkutano miaka yote na kupelekwa katika uwanja wa shule ya Azimio amesema kuwa uwanja huo kuanzia sasa utaitwa uwanja wa Salumu Mwalimu, alisema kuwa tukio hilo liliwahi kutokea na mkoani Mbeya katika uwanja wa sokoine na kuhamishiwa katika uwanja wa CCM ambao wanauita uwanja wa Dr. Slaa ambao miaka yote sasa wanafanyia mikutano huko.


Alisema kuwa Chama hicho hata kikifanyiwa visa na Jeshi la Polisi lakini kitajitahidi kupigania haki za wananchi wake na kuwa kita hakikisha mwaka huu kina chukua nchi.