MGOGORO uliokuwepo baina ya wananchi wa mtaa wa Ranadhani
halmashauri ya Njombe na mkandalasi wa umeme wa Umeme vijijini (Rea),
umemalizika ambapo wananchi walikuwa wanakataa kupitishwa umeme katika viwanja
vyao na sehemu wanazotaka kujenga.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Ramadhani
ulikukuw amgogoro baada ya kuonyesha eneo la kupitisha umeme unaoenda vijijini,
Meneja wa Tanesco mkoa wa Njombe, Eng Andrew Kichiwa, alisema kuwa wananchi walicho kuwa wakipingana
na Rea ni kupitishwa nguzo hizo katika makazi yao ambapo msanifu mradi
hakuzungumza na wananchi wakati wa kuweka mradi huo.
Alisema mgogoro huo umeisha baada ya wananchi kuonyesha
maeneo ambayo mradi huo unatakiwa kupita tofauti na ambapo ulitakiwa kupita
awali maeneo ambayo ni makazi yao na kuonyesha maeneo ambayo ni barabara za
mitaa na kupitisha umeme huo.
“Katika eneo hili wananchi walikuwa wanakataa kupita umeme
kutokana na msanifu wa mradi alipitisha umeme katika makazi yao na katika
hifadhi ya barabara kulikuwa nyumba za watu ambao wanatakiwa kulipwa fidia na
bado hawajalipwa na haijulikani watalipwa lini,” alisema .
Meneja aliongeza: “Mradi unamdawake wa kuisha umeme
unahitajika kupitishwa hivyo mgogoro umemalizwa kwa kuzungumza na wananchi na
kuonyesha sehemu ya kupita umeme,” aliongeza.
Kilicho leta mgogoro baina na wananchi kinadaiwa ni
ushirikishwaji wa wananchi wakati wa kuweka mradi huo ambapo wananchi
hawakutaka nguzo za umeme huo kusimikwa katika maeneo ambayo tayali wanaplani
za kujenga.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Ramadhani, Bathomeo
Kyando alisema kuwa mgogoro huo umetokana na kuto washirikisha wananchi wakati
wa uwekaji wa nguzo zizo na kuwa mgogoro huo hautajitokeza tena kwa kuwa
wananchi wenyewe wameonyesha eneo la kupita mradi huo.
“Tatizo hili lilijitokeza kutokana na ushirikishwaji wa
wananchi haukuwepo ndio maana kumekuw ana mgogoro na mkandalasi kupata kazi ya
kuweka na kutoa nguzo katika eneo hili lakini baada ya mazungumzo na wananchi
na wameonyesha maeneo ya kupita mradi hakutakuwa na mgogoro tena mradi utapita
bila kuw ana wasiwasi,” alisema Kyando.
Kwa upande wa wananchi walisema kuwa walishangaa kuona nguzo
zinawekwa katika maeneo yao ambayo wanatarajia kujenga baada ya kufukuzwa na
wakala wa barabara Tanzania (Tanroad) baada ya kulipwa fidia.
Walisema kuwa kwa maeneo ambayo wameonyesha umeme upiti
hawana pingamizi na umeme utapita bira ya kuwapo kwa matatizo yoyote na wao
wanafurahi kuona wenzao wanapata umeme lakini kwa kupitisha katika makazi yao
hawakufurahia.