Na Furaha Eliab, Njombe

MKUU wa mkoa wa Njombe Dtk. Rehema Nchimbi amewataka wakurugenzi wa halmashauri,wakuu wa Wilaya  pamoja na maafisa Mkoani hapo watakaofanyakazi ya kuwaandikisha wananchi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kusimamia vizuri zoezi hilo litakapoanza.


Dkt Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wazee na viongozi wa dini mkoani hapa juu ya tarehe rasmi ya kuanza kwa zoezi hilo hapo Februari 23 mwaka huu baada ya kuahilishwa Februari 16.

“Wakurugenzi, watendaji na mtakao husika katika zoezi hili mlifanye kwa ufanisi na mhakikishe linafanyika bili kupata dosali mpaka linanalizika, ili tuonyeshe upendeleo huu kuwa haujakosea kuja katika mkoa wetu huu,” alisema Dkt. Nchimbi.

Alisema kwa kuwa mkoa wa Njombe umekuwa wa kwanza katika zoezi hilo muhimu la kitaifa hivyo ni vyema viongozi hao kwa nafasi yao wakatumia vizuri fursa hiyo kutoa elimu kwa wananchi na waumini wao.

Aidha aliwataka wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari hilo la kudumu kwani bila kujiandikisha katika taftari hilo hawatakuwa na haki ya kupiga kura katika Kura ya maoni ya Katiba Pendekezwa na uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu.

Aidha Dkt. Nchimbi alisema zoezi hilo litaanzia ndani ya wilaya ya Njombe katika halmashauri ya mji wa Makambako hivyo ni vyema  kila mmoja akashiriki kikamilifu katika zoezi hilo vikiwemo vyama vya siasa.

“Zoezi hili linalo tarajiwa kuanza Februari 23 mwaka huu katika mkoa wetu huu litaanza katika halmashauri ya mji mdogo wa Makambako katika wilaya ya Njombe, kuhusi vifaa na vitu vingine tutawajuza kupitia vyombo vya habari na msiwe na wasiwasi kuhusu hilo,” alisema Dkt. Nnchimbi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba alisema atasimamia vizuri zoezi hilo katika wilaya yake pasipo kigugumizi chochote huku akiwaonya watu watakaoanza kupotosha umma juu ya zoezi hilo.

Nao wadau walio hudhulia katika mkutano huo wa mkuu wa mkoa walisema kuwa kuhusu vifaa wananchi wasiwe na wasiwasi na uvumi kuwa ni vichache kwa kuwa zoezi lenyewe bado halijaanza na kuwa wasuburi zoezi lianze ndipo zianza kutolewa lawama.

Mchungaji Alfred Mwagike wa Tanzania Assemblies of God (TAG), ni moja ya walio pata nafasi ya kuhuzuria zoezi hilo na aliwataka wananchi kuacha na uvumi wa kuwa zoezi hilo litagubikwa na uchache wa vifaa hivyo wajitokeze katika zoeli hilo bila kusitasita na wajiandikishe ili wapate sifa ya kupiga kura na kupata kitambulisho ambacho kimekuwa kikitumika katika shughuli mbalimbali.