JUMUIYA ya wafanyabiashara mkoani Njombe imesema itaenda Mahakamani kuweka
msimamo wa kukataa tozo la kodi la asilimia 100 kutoka serikalini kupitia
mamlaka ya kukusanya  mapato Tanzania TRA kwa madai kuwa ongezeko hilo
limekuwa kubwa ikilinganishwa na hali ya biashara katika maeneo mbalimbali

Jumhia hiyo pia imekubaliana kuwaunganisha wafanyabiashara wakubwa na
wadogo ili kutekeleza malengo mbalimbali ikiwemo kuziba myanya ya rushwa
baina ya wafanya biashara na maofisa wa TRA wasio waaminifu ambao wamekuwa
wakiwatisha wafanuyabiashara  na kisha kupokea rushwa badala ya kukusanya
kodi ya serikali kama inavyo paswa

Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa jumiya hiyo mjini makambako
Mwenyekiti wa Korido ya wafanyabiashara Mkoa wa Njombe (Tccia), Oraph Mhema
 Amesema kuwa wafanyabiashara weameazimia kwenda mahakamani kupinga
ongezeko la kodi baada ya kugundua kuna ongezeko la asilimia 100 wakati wa
kulipia mapato ambapo maafisa TRA Wameshindwa kutoa ufafanuzi sahihi pindi
wanapo ulizwa

Kwa upande wake mwakilishi wa mwenyekiti wa jumhia ya wafanyabiashara taifa
jaohn minja bwa Charles Syonga amesema kuwa   jumhia hiyo imepata  baraka
za kuundwa kutoka kutoka kwa baadhi ya viongozi wakubwa serikali akiwemo
waziri mkuu mizengo pinda lengo lake si kupinga wafanyabiashara kulipa kodi
bali ni kutafuata misingi ya haki baina ya serikali na wafaanya biashara

Kuhusu mashine za kielektroniki EFD amesema kuwa wamebaini kuwa zina
mapungufu makubwa na hazitumiki popote duniani bali Tanzania na zinakasoro
nyingi ikiwemo kutokuwa na sehemu ya kufuta makosa yanapojitokeza pamoja na
kutilia shaka kuwa huenda ukawa ni mradi wa kikundi fulani cha watu
kutokana na kuto kuwa na bei sahihi elekezi

Katika mkutano huo kumefanyika uchaguzi wa viongozi wa jumhia ya
wafanyabiashara halmashauri ya mji wa makambako tofauti na ilivyotarajiwa
awali kufanyika uchaguzi wa jumhia mkoa kutokana na wafanyabiashara wa
kutoka wilaya za mkoa wa njombe ikiwemo  njombe mjini kutohudhuria mkutano
huo ambapo Sifaeli sigala amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumhia hiyo ya
wafanyabiashara halmashauri ya mji wa makambako