Askali ahukumiwa miaka 30 Jela

ASKALI aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumbaka mahabusu katika kituo kidogo cha Polisi Ilembula wilaya ya Wanging’ombe mkoani hapa Juma Nyambega ametupwa jela miaka 30 baada ya mahakama ya Hakimu mfawidhi Njombe kuridhika na ushahidi uliotolwa mahakamani hapo.

Askali huyo aliyekuwa anafanyakazi katika kituo kidogo cha Polisi Ilembula wilayani Wanging'ombe  mkoani hapa mweye namba F 6565 Nyambega juzu mahakama ya hakimu mkazi Njombe mbele ya hakimu Mkazi mfawidhi Augustine Rwezile alihukumiwa kwenda jela miaka 30.

Akisoma hukumu hiyo Juzi Rwezile alisema  mahakama imerizika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mlalamikaji pamoja na vielelezo vya daktari aliyempima binti huyo mwenye umri wa miaka 19 na kubaini kuwepo kwa michubuko sehemu zake za siri.

Askali huyo alipandiswa mahakamani hapo kwa kosa la kumbaka binti mahabusu ambaye alikuw ana umri wa miaka 19 ambapo inadaiwa alitolewa katika chumba chake cha mahabusu na kumbaka.

“Mahakama baada ya kusikiliza maelezo ya daktari aliye mpima biti huyo na maelezo ya upande wa ulalamikali umebaini kuwa mshitakiwa alifanya kosa hilo na mahakama inamhukumu mshitakiwa kwenda jela miaka 30” alisema Rwenzile.

Aidha hakimu Rwezile alisema kuwa mtuhumiwa huyo atakwenda  jela miaka 30 kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 130 kifungu kidogo cha kwanza  na cha pili  A na cha 35 B pamoja na kifungu cha 131 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya kanuni ya adhabu   sura ya 16 kama ilivyo  rejewa mwaka 2002.

Alisema kuwa mshitakiwa kama atakuwa hajarizika na maamuzi ya hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama yake anaruhusiwa kwenda kukata rufaa.

Awali akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali Magdalena Kisowa  aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa  huyo alitenda kosa hilo mnamo  mei 10  2014   majira ya saa mbili usiku   akiwa kituo cha polisi  Ilembula ambapo alikwenda kwenye chumba cha mahabusu ambacho alikuwepo  mlalamikaji  huyo na kutekeleza tendo hilo la ndoa kwa kutumia nguvu.

Aliongeza kuwa mshitakiwa, alikwenda kutoa kwenye chumba  cha mahabusu alicho kuwemo mlalamikaji na kusema anampeleka chumba kingine ambacho kilikuwa na mwanga na kisha kufanya tendo hilo la udhalilishaji.

Aidha wakili Kisowa aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa m shitakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za ubakaji kwani kitendo hicho ni cha unyanyasaji  na  udhalilishaji kwa  mwanamke.