Mwanamke mmoja mkazi wa kata ya Buhare katika manispaa ya Musoma mkoani Mara Bi.Helena Paulo mwenye umri wa miaka 20 amejifungua watoto wawili mapacha ambao wameungana katika eneo la kifua hadi tumboni tukio ambalo limevuta mamia ya wananchi ambao wamefika katika Hospitali ya rufaa mkoa wa Mara mjini Musoma kwa lengo la kutaka kushuhudia tukio hilo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa mara mjini ,Musoma,muuguzi wa zamu Bi. Naabu Geraruma,amesema kuwa mwanamke huyo amefanikwa kujifungua usiku wa saa saba kuamkia leo Jumatatu kwa njia ya operesheni watoto hao wawili wenye jinsi ya kike huku wakiwa na uzito wa kilo
4.6
Hata hivyo muuguzi huyo wa zamu amesema tukio hilo ni la kwanza kutokea katika Hospitali ya mkoa wa Mara na kwamba hali za mwanamke huyo na watoto zinaendelea vema na taratibu za kumpeleka hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza zimekamika.
Hata hivyo mkurugenzi wa utawala na rasmali watu wa hospitali ya rufaa ya Bugando Bi.Leah Kagine amesema tayari mwanamke huyo na watoto wamefikishwa katika hospitali ya rufaa kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
via>>ITV