Wataalam JWTZ kuchunguza bomu lililolipuka Singida.

Akieleza zaidi kamanda Sedoyeka amesema baada ya kupeleka zawadi hiyo nyumbani kwake aliyo pewa siku ya tarehe thelasini mwezi wa kumina mbili mwaka jana na kuamua kuifungua tarehe mbili mwezi wa kwanaza mwaka huu na kulipuka, ulikuwa na ujumbe unaosema hatuwezi kufana dili ya shilingi milioni tisini na kutuzurumu.

Jeshi la polisi mkoani Singida limeamua kuagiza wataalamu wa mabomu kutoka jeshi la wananchi mkoani Arusha kwa ajili ya kuchunguza na kubaini kitu ambacho kinasadikiwa kuwa bomu ambalo lilimlipukia mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Bi.Halima Mpita.

Akieleza kwa waandishi wa habari huku akionyesha mabaki ya bomu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema tukio hilo ambalo limetokea siku ya tarehe mbili mwezi wa kwanza, baada ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Bi Halima Mpita kupewa zawadi ya mwaka mpya kutoka kwa katibu mutasi wake iliyo ipokea kutoka kwa wadau wake.
Jeshi la polisi mpaka sasa bado hawajafanikiwa kumshika mtu aliye husika na tukio hilo na uchunguzi zaidi unaendelea, ili kuweza kuwabaini walio husika na kuchukuliwa hatua kali za sheria