Saccos ya vijana Wanging'ombe, Yazinduliwa





VIONGOZI wa msakosi hapa nchini wametakiwa kutazama kwa umakini michanganuo ya wanachama wao wanao hitaji mikopo ili kukabiliana na tatizo la kuwapo kwa watu wanao shindwa kulipa malejesho ya mikopo yao.

Hayo yamebainishw ana mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe wakati wa uzinduzi wa Saccos ya Vijana Ulembwe Saccos limited ya wilayani humo, alisema kuwa uongozi wa saccos uangalie kwa makini mchanganuo kwa lengo la kukupisha mtu anayeweza kurejesha mkopo.

Alisema kuwa kumekuwa na matatizo ya kuto rejeshwa kwa mikopo katika saccos nyingi hapa nchini kutokana na wakopaji kuto kuwa na michanganuo sahihi wa pesa anayokopa.

“Watu wengi wamekuwa wakikopa kwa kuangaliwa mwenzake kachukua fomu ya mkopo basi nae anachukua lakini unakuta mtu hana malengo ya mkopo na wengine wanakopa pesa zaidi ya lengo lake na kushindwa kurejesha,” alisema Kilasi
Alisema kuwa asilimia kubwa ya wananchi wamekuwa wakijiingiza katika mikopo kwa kuiga na kujikuta wakibadilisha sehemu za kukopa kwa kulipa madeni katika saccos za awali.

Kwa upande wao wananchi na viongozi wa Kijiji Cha Ulembwe ambapo ndio makao makuu ya sakosi hiyo wamewataka vijana kujiunga katika vikundi mbalimbali zikiwemo sakosi ili kuweza kusaidiwa na serikali katika mikopo yake kwa vijana.

Katibu wa saccos, Nebchard Msigwa alisema kuwa kupitia hapo wataweza kuwakopisha vijana hasa zile pesa za serikali zilizo tengwa kwajili ya vijana na wanawake kwa kuwa hapo ni sehemu ambayo ni salama na inaaminika kama anavyo eleza.

Afisa mtendaji wa kijiji cha Ulembwe, Peter Luhasi aliwataka wananchi hao waliojiunga katika saccos hiyo na kupata mkopo wa pembejeo za wakati wa uzinduzi wakawe mabarozi wazuri kwa wenzao ili nao wajiunge.

Naye diwani wa kata hiyo, Agneta Mpangile alipongeza juhudi za wananchi waliojiunga na saccos hiyo na kunufaika na matunda ya pesa wanazo weka kwa kupata mkopo wa pembejeo.

Kwam muda wa mioezi sita wamefanikiwa kuweka pesa zaidi ya milioni 4 hivyo wakiendelea hivyo wanaweza kufika mbali na kuinua uchimi wao kwa kukopeshana.

Aidha mkuu wa chuo cha maendeleo ya Wananchi, Yohanes Chongolo alihimiza wananchi kujitokeza kujiunga ili kuunganisha nguvu katika saccos kwa kuwa kwa mwananchi wa sasa bila kukopa hawezi kufanya maendeleo thabiti lakini wakiunganisha mitaji yao wataendelea kwa kukopeshana.